Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video : Utani Kati ya Samsung na Apple Bado Unaendelea..

Nani zaidi kati ya Samsung Galaxy S9 na iPhone X…?
utani wa jadi utani wa jadi

Ni kweli kwamba soko la simu janja (smartphone) linazidi kuwa gumu sana kadri siku zinavyokwenda, pengine hii inatokana na kuwepo kwa kampuni nyingi zinazo chipukia kama OnePlus na nyingine ambazo ukweli zinakuja kwa kasi sana. Sasa kwa upande wa makampuni haya makubwa njia pekee iliyobaki ili kuongeza mauzo ni kupitia ubunifu na utani wa jadi.

Wote tunajua utani kati ya Samsung na Apple haujaanza leo, kumekuwa na kesi, utani na ubishani mkubwa baina ya wateja na pia baina ya makampuni haya makubwa ya utengenezaji wa simu. Kama ulifanikiwa kupata habari hivi karibuni Samsung na Apple walifikia hatua ya hitimisho baada ya kesi yao iliyokuwa ikiendeshwa kwa muda wa miaka 8 kufikia hatua ya maamuzi kwa Samsung kuilipa Apple zaidi ya dollar za marekani milioni $538.

Advertisement

Sasa baada ya maamuzi haya kilichobakia pekee ni utani kati ya kampuni hizi mbili huku kila mmoja akijinadi kuwa bidhaa zake ni bora zaidi.. Angalia video hapa chini.

Kama unataka ufafanuzi kidogo kuhusu tangazo hili ni kuwa, kwenye tangazo hili mteja alikuwa anataka kujua kuhusu ubora wa speed ya kudownload kati ya Samsung Galaxy S9 na iPhone X, na  kwa sababu Galaxy S9 inaspeed kubwa ya kudownload kuliko iPhone X, muuzaji wa duka la Apple anakosa la kusema na inakuwa mwisho wa Tangazo.

Sasa tukija upande wa ufafanuzi wa kiteknolojia, Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, Galaxy S9 ina kasi ya kudownload mara mbili zaidi ya iPhone X huku S9 ikiwa na kasi ya kudownload hadi MB 100 kwa sekunde, wakati iPhone X ikiwa na kasi ya kudownload hadi MB 50 kwa sekunde.

Hii sio mara ya kwanza kwa Samsung na Apple kutaniana kuhusu uwezo wa simu zao, unaweza kusoma hapa ili kuona utani mwingine wa jadi baina ya kampuni hizi mbili. Pia kama unataka kujua simu ipi ni bora kati ya Galaxy S9 na iPhone X unaweza kusoma hapa kujua simu ipi zaidi.. Je wewe ni Team Galaxy au Team iPhone tuambie kwenye maoni hapo chini…

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use