Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta

Utaweza kutumia simu yako kama imeharibika kioo au kama kioo hakifanyi kazi
Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta
©123rf.com

Ni wazi kuwa simu za Android zina nunuliwa zaidi kuliko simu nyingine kama iPhone na nyingine, lakini ni wazi kuwa pia simu za Android ni moja kati ya simu ambazo zinaharibika kwa wingi.

Kuliona hili leo nimekuleta makala ambayo binafsi naamni inaweza kukusaidia sana hasa pale simu yako ya Android inapo haribika. Kumbuka kuwa njia hii inafanya kazi kwenye simu yoyote ya Android bila kujali toleo la Android au aina ya Brand unayo tumia.

Advertisement

Kwa kusema hayo basi moja kwa moja twende nikakuonyeshe sehemu ambayo ni muhimu kuwasha kwenye simu yako Android pale tu unapo inunua.

Washa Sehemu hii Unapo Nunua Simu ya Android.?

Najua ni wazi kuwa unajua moja ya sehemu ambayo huharibika sana kwenye simu za Android ni “Kioo”, na pia moja kati ya sehemu ambayo inatumia gharama kubwa kutengeneza ni kioo. Kwa kurekebisha kioo kwenye simu ya Android unaweza kujikuta unatumia gharama sawa na simu mpya hivyo pengine ni bora kununua simu mpya kuliko kubadilisha kioo.

Sasa hapa swali linakuja, Je unawezaje kutoa vitu vilivyopo kwenye simu yako na kioo cha simu yako hakionyeshi au hakibonyezeki..?

Kukupa jibu ya swali hili ndio maana leo nimekuletea makala hii ambayo itakusaidia kutumia simu yako ya Android hata kama simu yako imeharibika kioo. Hii itakusaidia kutoa vitu vyako kwenye simu ikiwa pamoja data zako muhimu.

Tumia Simu Kama Kioo Kimeharibika

Sasa mtu yoyote mwenye simu ya Android anaweza kutumia simu yake pale inapo haribika kioo, unaweza kufuata hatua zifuatazo kuwasha sehemu ambayo itakusaidia kutumia simu yako pale kioo kitakapo pata shida.

Kwa kuanza chukua simu yako ya Android kisha bofya sehemu ya Settings > Kisha Software Information au System, kisha tafuta tafuta About Phone au moja kwa moja tafuta sehemu ili andikwa Build Number.

Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta

Baada ya kufika kwenye sehemu ya Build Number bofya mara kumi (10) kwenye sehemu hii hadi uone maneno yakitokea yenye kuonyesha kuwa “Developer Mode” imewezeshwa.

Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta

Baada ya hapo moja kwa moja rudi kwenye uwanja wa Settings na utakuta sehemu mpya ya Developer options.

Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta

Kupitia sehemu hii moja kwa moja tafuta sehemu ya USB debugging kisha hakikisha sehemu hii imewashwa na endelea kwenye hatua zifuatazo.

Tumia Simu Iliyopasuka Kioo Kupitia Kompyuta

Baada ya kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja utakuwa karibu kutumia simu yako iliyo haribika kioo au ambayo haifanyi kazi vizuri kwenye kioo. Kumbuka hatua hizi ni muhimu kufanya kama kabla ya kuendelea kwenye makala hii.

Hatua Nyingine Muhimu

Baada ya kufanya hatua hapo juu hatua zinazofuata ni muhimu na ni lazima kuwa na kompyuta ili kuweza kutumia simu yako kama kioo cha simu yako kime haribika au kama hakifanyi kazi.

Hatua ya kwanza ya muhimu ni kupakua programu hapo chini, programu hii ni ya bure kabisa na pia ni Open Source hivyo unaweza kuimiliki kwa asilimia 100 bila kujali malipo ya aina yoyote.

Download File Hapa

Baada ya kudownload programu hiyo Extract file hizo kwenye kompyuta yako ndani ya file moja kisha fungua ndani ya file hilo na tafuta file ambalo limeandikwa “scrcpy.exe” na kisha bofya mara mbili huku simu yako ikiwa imechomekwa kwenye kompyuta.

Kama unavyoweza kuona umuhimu wa sehemu hiyo ni kuwa utaweza kutoa vitu vyote kwenye simu yako kwa haraka na bila kutumia muda mrefu. Kumbuka kuwa ni lazima kufanya hatua zote moja baada ya nyingine ili kuweza kufanikisha hili.

Pia ni muhimu sana kuwasha sehemu hii ya USB Debugging kwani itakusaidia sana kwenye mambo mengi pia hata kama umesahau pattern kwenye simu yako ya Android.

Kama umefurahia makala hii basi unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech hapa kuweza kujifunza zaidi mambo mbalimbali kwa vitendo, pia tunategemea kufanya maboresho mengi pamoja na kuja na makala mpya zaidi hivyo endelea kutembelea channel ya Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use