Wanasayansi kutoka nchini marekani hivi karibuni wamefanikiwa kukuza kiumbe hai (kondoo) kwenye kifaa maalumu yaani nje ya tumbo la uzazi. Wanasayansi hao wamefanikiwa hilo baada ya kumuweka kondoo ambaye anaendelea kukuwa vizuri ndani ya kifaa hicho huku sehemu za mwili wake kama ubongo pamoja na sehemu zingine za mwili zikionyesha kukua vizuri.
Wanasayansi hao wanasema kwa kutumia kifaa hiki chenye mfano wa lailoni lenye maji ya uzazi (Biobag), pengine kitaweza kusaidia kwenye miaka ya karibuni kukuza hata binadamu nje ya tumbo la uzazi. Wanasayansi hao bado wanaendelea na uchunguzi wao wakati kondoo huyo akiendelea kukua vizuri kwenye kifaa hicho maarufu kama Biobag.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.
Nimeipenda sana blog hii daah vizuri sana