Wanasayansi katika chuo cha Drexel University’s College of Engineering cha huko Philadelphia, Pennsylvania wako kwenye hatua za awali za kutengeneza battery yenye uwezo wa kujaa kwa haraka.
Wanasayansi hao wame-sema wana matumaini ya kufanikisha hilo kutokana na majiribio ambayo wanafanya sasa kwenye aina ya material ambayo inaitwa MXene material. Material hiyo sio mpya kuisikia bali wanasayansi hao wamefanyia uchunguzi zaidi na kuweza kubaini njia hiyo ya kutengeneza battery zenye uwezo wa kujaa kwa haraka.
Uchunguzi huo ambao umefanyika na watalamu hao umebaini kuwa material hiyo inauwezo wa kufungamana kwa haraka hivyo kusababisha uwezo wa kujaa kwa chaji uwe wa haraka zaidi pengine chini ya dakika moja.
Hata hivyo wanasayansi hao wamesema ugunduzi huo hauta ishia battery za simu pekee hii itaenda mpaka kwenye battery za magari pamoja na vifaa vingine vinavyo tumia battery, wanasayansi hao kwa sasa wako kwenye hatua za awali za ugunduzi huo na wamesema pengine hadi kufikia mwaka 2020 battery hizo zitakuwa tayari kwa matumizi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Chanzo : The Next Web