Kuna wakati unataka kujua ni app gani ambazo umetumia sana kwa siku nzima, iwe wewe ni mpenzi wa Instagram, TikTok au unataka kujua ni app gani ambazo mtu ametumia baada ya kushika simu yako.
Kupitia njia hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia wallpaper kujua ni app gani ambazo zimetumika sana kwenye simu yako, njia hii ni rahisi na mtu yoyote anaweza kufanya kwenye simu yoyote ya Android. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.
Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload fungua app hiyo kisha endelea kwa kufuata maelezo hapo chini.
Kwa kuanza kubali vigezo na masharti kisha moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa unafuata ambapo unatakiwa kubofya sehemu ya Go to settings.
Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambapo unatakiwa kuwasha app hii kupitia sehemu ya data acces bofya kutufe kuwasha app hii.
Baada ya hapo bofya kufe cha kurudi nyuma na utapelekwa kwenye ukurasa ambapo unatakiwa kuchangua wallpaper ambayo unapendezwa nayo.
Zipo wallpaper tatu tu ila hizi ndizo zenye uwezo wa kufanya maajabu niliyo kwambia, changua wallpaper unayotaka kwa kubofya view. Kama umependa muonekanao wa wallpaper hiyo moja kwa moja bofya set wallpaper.
Baada ya hapo bofya sehemu ya mwisho ambayo ni Set wallpaper ambayo ipo mwisho kabisa kwenye simu yako, kisha baada ya hapo chagua unataka kuweka wapi wallpaper hiyo kati ya Home screen au Home screen and lock screen.
Baada ya hapo utaona wallpaper hiyo ikiwa imewekwa moja kwa moja, sasa unaweza kuendelea kwenye kutumia simu yako na utaweza kuona ni app gani unazo tumia sana kwenye simu yako kwa kubofya kioo cha simu yako na utaona maandishi yakitokea kwenye kila chumba.
Kadri chumba kinavyo zidi kuwa kikubwa ndipo inapo onyesha kuwa unatumia app hizo kwa wingi kuliko app nyingine.
Kwa kutumia njia hii natumaini utakuwa umejua ni app gani uzaotumia kwa wingi kwenye simu yako, kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kubadilisha simu yako kuwa na muonekano kama wa iPhone 12. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea Tanzania tech kila siku.