Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Picha : Wagunduzi wa Teknolojia Kabla na Baada ya Kufanikiwa

Wagunduzi wa Teknolojia mbalimbali kabla ya kuwa maarufu
Wagunduzi wa Teknolojia Wagunduzi wa Teknolojia

Habari ya jumapili ya leo mwana teknolojia najua, leo ume pumzika hivyo sita kuchosha kwa makala ndefu na maneno mengi. Makala hii ya leo ina lengo moja kubwa sana kwenye maisha ya kila siku ikiwa ni kuhimiza “kutokata tamaa kabisa kwenye maisha haijalishi uko wapi kwa wakati huu”.

1. Jeff Bezos, Mgunduzi wa Kampuni ya Amazon Mwaka 1999

Advertisement

Kwa wale ambao hamjui, Jeff Bezos ndio mgunduzi wa kampuni na tovuti ya Amazon.com ambayo hivi karibuni imezindua duka lisilo na muuzaji la Amazon Go. Kwenye picha hapo ni miaka 18 nyuma wakati Jeff akiwa anafanyia kazi wazo lake na kwa sasa jamaa ana utajiri wa dollar za marekani bilioni $118.8 na alishawahi kuwa tajiri wa dunia kwa muda mfupi kwa kumshinda Bill Gates.

2. Mark Zuckerberg Akifanyia Kazi Tovuti ya  Kwanza ya Facebook

Wote tunajua historia ya Facebook pamoja na mwazilishi wake Mark Zuckerberg, lakini kwenye picha hapo juu ni wakati Mark akiwa chuoni pamoja na wenzake wakifanyia kazi tovuti ya kwanza kabisa ya Facebook amabyo kipindi hicho ilikuwa inaitwa thefacebook.com. Kwa sasa wote tunajua utajiri alionao jamaa huyu, Jamaa ana utajiri  zaidi ya dollar za marekani bilioni $76.7.

3. Larry Page na Sergey Brin Waanzilishi wa Google

Larry Page na Sergey Brin wanzilishi wa kampuni na tovuti ya Google ambayo sasa inamiliki mitandao inayo tengeneza pesa kila siku. Picha hapo juu ni wakati wakiwa wanafanyia kazi tovuti ya Google. Larry Page na Sergey walikutana chuoni stanford na wazo la Google ndilo liliwaunganisha na kuwa marafiki. Kwa sasa Larry page ana utajiri wa zaidi ya dollar za marekani bilioni $51.7 na Sergey Brin anautajiri wa dollar za marekani bilioni $50.3.

4. Jerry Yang na David Filo Wazilishi wa Yahoo

Jerry Yang na David Filo ni waanzilishi wa mtandao wa Yahoo ambayo ndio kampuni ya kwanza iliyokuwa inategemewa sana kwa barua pepe, waanzilishi hawa kama walivyo waanzilishi wa Google walikutana chuoni na hatimaye urafiki wao ulizaa wazo hilo la Yahoo. Kwa sasa Jerry Yang ana thamani ya dollar za marekani bilioni $2.7 huku David Filo akiwa na thamani ya dollar za marekani bilioni $5.5.

5. Steve Jobs Mgunduzi wa Kampuni ya Apple

Kwenye picha mtu wa tatu kutoka kulia ni Steve Jobs, hapo alikua yupo shule kwenye darasa la kujifunza electroniki, mbali na kugundua Apple Steve Jobs alisha kugundua na kumiliki kampuni nyingi kabla ya hapo ikiwa pamoja na kampuni ya NeXT pamoja na kampuni ya filamu ya Pixar. Hadi kufikia mwaka 2011 Steve Jobs alikuwa na utajiri wa dollar za marekani bilioni $10.2.

BONUS

Kwa sababu leo ni jumapili na ni siku ya je wajua, labda nikuache na hili pia nje ya teknolojia. Hivi unajua kuwa mwana muziki rihanna alikuwa mwanajeshi tena mwenye cheo cha koplo kabla ya kuwa mwanamuziki..? Sidhani kama alitegemea kuwa mwanamuziki kwenye kipindi hichi, (Rihanna wa pili kutoka kulia).

Na huu ndio ushauri wa picha nilio kuandalia leo, ukweli ni kwamba kwenye nia pana njia haijalishi uko wapi sasa, muhimu ni kuendelea kufanyia kazi ndoto zako hata kama uko na hali gani kwa sasa cha msingi ni kusonga mbele na kuto kukata tamaa. Labda siku moja tutakuja kuandika hapa kwa ugunduzi utakaoufanya.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use