Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Wafanyakazi 50 wa Apple Waacha Kazi Kwaajili ya Kifaa Hichi

Wafanyakazi wa Apple 50 wameamua kuacha kazi sababu hii..
Wafanyakazi wa Apple Wafanyakazi wa Apple

Kumekua na tetesi za hapa na pale kuhusu kampuni ya Apple kuwa na mpango wa kutengeneza programu kwaajili ya magari yanayo jiendesha yenyewe, tetesi hizo pia zinasema kuwa kuna uwezekano pengine kampuni hiyo ikamua kutengeneza magari hayo kabisa.Hata hivyo tetesi hizo zinasema kampuni ya Apple ilikua kwenye hatua za mwanzo za kujiandaa kwa kuongeza wataalamu zaidi kwenye upande wa magari.

Lakini katika hali ya kushanga wataalamu takriban 50 walio tegemewa kutengeneza programu au magari hayo wameamua kuacha kazi kutoka kampuni ya Apple na kuungana na kampuni mpya ambayo imegundua kifaa ambacho kinakusaidia kuweza kuona pale unaporudisha nyuma gari lako. Kifaa hicho ambacho kimetengenezwa na kampuni ya Pearl Auto hakiitaji gari la kisasa bali , utakifunga kwenye gari lolote na moja kwa moja kitaonyesha Video ya HD pale unaporudi nyuma kwa kupitia simu yako ya mkononi.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya habari za teknolojia, wafanyakazi hao walionekana kutaka kujiunga na kampuni hiyo mapema kwa kile kilichosemekana kuwa walitaka kutengeneza teknolojia ambayo itadumu kwa muda mrefu kuanzia sasa na sio magari yanayojiendesha ambayo kwa sasa bado yanafanyiwa majaribio.

Kifaa hicho kipya cha Pearl RearVision Wireless Car Backup Camera and Obstacle Alert System kwa sasa kinapatikana kupitia Amazon na unaweza kukinunua kwa dollar za marekani $499.99 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,200,000. Pia kifaa hicho kina sifa za kutokuingia maji (Water resist) , uwezo wa kutoa mlio (Alarm) pale kamera hizo zinapo ona kitu, uwezo wa kuonyesha usiku (Nightvision) pamoja na uwezo wa kutumika bila waya (Wireless).

Kwa habari zaidi za teknolojia tembelea Youtube Channel yetu au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka pindi zitakapo toka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use