Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi Wadukuzi Walivyoiba Bilioni 21 Kenya Mwaka 2017

Mwaka jana Kenya ilipoteza dola milioni 50 kwa wadukuzi
wadukuzi wadukuzi

BBC Swahili imeripoti kuwa, dola za Marekani milioni 210 ziliibwa na wadukuzi kutoka kwenye Benki na Taasisi za serikali nchini Kenya mwaka 2017. BBC imesema hii ni kwa mujibu w ripoti ya shirika la usalama mitandaoni, SERIANU, ambayo inasema mataifa ya bara la Afrika yalipoteza jumla ya dola milioni 350.

Hata hivyo BBC imeandika kuwa, ikizingatiwa kwamba, kati ya mwezi Januari na mwezi Februari mwaka jana, Kenya ilipoteza dola milioni 50 kwa wadukuzi, ni wazi kwamba usalama wa fedha za wateja wa benki haujazingatiwa na benki nyingi.

Advertisement

Akiongelea jinsi Udukuzu huo unavyotokea Delano Kiilu, ambaye ni mtaalam wa maswala ya usalama alisema kwa BBC Swahili kuwa, Kila siku wadukuzi wanabuni njia mpya za kudukua mifumo ya usalama mitandaoni huku benki zikisalia nyuma hatua moja. Kulingana na bwana Delano, 70% ya udukuzi unafanikishwa na wafanyikazi kwenye benki pamoja na wateja na asilimia 30% unatokana na wadukuzi kugundua mianya kwenye mifumo ya usalama kwenye banki.

Wadukuzi wengi wanatumia mbinu tofauti ikiwemo, kutuma ujumbe wa barua pepe unaowavutia wafanyakazi na wanapofungua wanawezesha wadukuzi kupenya kwenye mitandao ya benki hizo. “wafanyakazi wanatoa maelezo muhimu na ya siri kwa wadukuzi na kurahisisha wizi huo una baadae wizi huo kugundulika muda mrefu baada ya kufanyika”. Anasema bwana Delano kwa BBC.

Hata hivyo BBC iliandika kuwa sababu zinazosababisha mabenki kutokutoa taarifa pindi udukuzu huu unapotokea ni pamoja na Benki nyingi zinaogopa kupoteza wateja iwapo zitatangaza hadharani kwamba zimeshindwa kulinda pesa na maelezo ya wateja, na pia hii itasababisha Hofu kubwa na kusababisha wateja kujiondoa mara moja kwa wingi na kusababisha benki kufungwa.

“Nadhani wakati umefika kwa benki kuwafahamisha wateja wake kuhusu upungufu uliopo kwenye mifumo ya usalama na kufafanua jinsi wanavyokabiliana na tatizo hilo”. Anasema bwana Ali Khan Sachu ambaye ni mtaalamu wa maswala ya benki.

Kulingana na Fredrick Kirui, mkurugenzi mkuu wa mtandao wa mauzo mitandaoni AfrikaSokoni, maelezo binafsi ya wateja sio salama. “Mitandao mingi kimataifa na hususan barani Afrika inakabiliwa na changamoto ya wadukuzi wanaobobea kila siku”. Anasema bwana Kirui.

Bwana Kirui hata hivyo anawataka wateja kuwa waangalifiu wakati wananunua bidhaa mitandaoni ama wanapopeana habari binafsi kwa kampuni za mitandaoni, kwani maelezo hayo yanatumika kuwaibia pesa na pia kuwashawishi mitandaoni.

Imenakiliwa kutoka BBC Swahili na Kuhaririwa na Tanzania Tech

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use