Wengi tunajua tofauti iliyopo baina ya Korea Kasikazini na Korea Kusini lakini je unajua kuwa hivi karibuni wadukuzu wa korea kaskazini wamejulikana kuwa ni moja kati ya kichocheo cha ugomvi wa mataifa hayo jirani.?
Habari kutoka mitandao mbalimbali zinasema kuwa hapo mwezi Septemba mwaka jana Wadukuzi kutoka Korea Kaskazini walidukua mitambo ya kijeshi ya Korea Kusini na kuiba nyaraka nyingi zenye taarifa muhimu za kijeshi za korea kusini.
Aidha ripoti hiyo inasema kuwa Miongoni mwa yaliyokuwemo kwenye nyaraka hizo za siri za korea kusini ni pamoja na mpango wa kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un pamoja na nyaraka nyingine za muhimu kati ya korea Kusini na Marekani.
Hata hivyo taarifa hiyo ilitolewa na Korea Kusini mwezi mei huku ikifichua kwamba sehemu kubwa ya data iliibiwa na wadukuzi wa korea kaskazini Septemba mwaka jana, madai ambayo Korea Kaskazini ilikanusha.
Jeshi la Korea Kusini limesema kufikia sasa asilimia 80 ya taarifa ambazo ziliibiwa kufuatia udukuzi huo bado hazijatambuliwa.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa ha
Chanzo : BBC Swahili