Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Vodacom Tanzania Yaja na Ofa ya Bonge la Bando

Bando hilo linatoa GB 1 kwa Tsh 1000, na dakika 300 kwa Tsh 1000
Kampuni ya Vodacom Tanzania Yaja na Ofa ya Bonge la Bando Kampuni ya Vodacom Tanzania Yaja na Ofa ya Bonge la Bando

Kampuni inayotoa huduma za simu ya Vodacom Tanzania, hivi karibuni imetangaza ujio wa ofa yake mpya inayo julikana kama bonge la bando. Ofa hiyo imetangazwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi.

Hata hivyo bonge la bando imetangazwa wakati mkurugenzi huyo Alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampeni yao mpya ya Mtandao Supa, yenye lengo la kuongeza ufahamu kwa wateja kuhusu mtandao wake wenye ubora wa hali ya juu na manufaa makubwa yanayopatikana kwa wateja wake kupitia mtandao huo.

Advertisement

Kampuni ya Vodacom Tanzania Yaja na Ofa ya Bonge la Bando

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, mkurugenzi huyo alisema, “kupitia kampeni hii wateja wa Vodacom watajipatia bando mpya maalum inayoitwa Bonge la bando ambayo ina thamani hadi mara tano ya walicholipia”.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Bi Linda Riwa alisema ili kuwaruhusu wateja wao kupata nafasi ya kufurahia kampeni hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua ofa hiyo mpya ambayo inatoa unafuu kwa mteja kutumia sauti na data kwa bei rahisi.

Jinsi ya Kujiunga na Bonge la Bando

Jinsi ya kujiunga wateja wa Vodacom wata jisajili kwenye bando hii kwa kupiga *149*01# kisha chagua Internet kama unataka Data, au Chagua Cheka kama unataka kujiunga na dakika. Bando hilo linatoa GB 1 kwa Tsh 1000, na dakika 300 kwa Tsh 1000 kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku.

Kwa sasa tayari ofa hii inapatikana kwa kila mteja anae tumia mtandao wa Vodacom Tanzania,  unaweza kupata ofa hiyo moja kwa moja kwa kupitia Menu hapo juu. Pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Songesha ya Vodacom Tanzania.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use