Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Kuleta Baadhi ya Vipengele vya Note 7 kwenye Galaxy S 7

Hii ni kwa wapenzi wa Samsung Note 7 sasa utapata baadhi ya vipengele vya Note 7 kwenye samsung S 7
note note

Hivi karibuni kampuni ya samsung ilitangaza rasmi kuachana na utengenezaji wa simu zake za Note 7 hivyo wateja wote wenye simu hizo walilazimika kubadilisha simu hizo au kurudisha simu hizo ili kupewa simu nyingine. Hata hivyo baadae samsung ilitangaza rasmi kutoa fidia ya kiasi cha dollar za marekani $100 kwa wateja ambao wataendelea kutumia simu kutoka kampuni hiyo pale watakapo rudisha simu hizo za Galaxy Note 7.

Ili kuendelea kuwaridhisha wateja wake Samsung imeanza kutoa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa Simu za Samsung Galaxy S7 ambao utakua na baadhi ya vipengele (Features) ambavyo vilikwepo kwenye simu ya Samsung Galaxy Note 7. Tayari baadhi ya wateja wamesha anza kupata toleo hilo jipya ambalo lina vipengele hivyo ambavyo ni pamoja na vipengele vya kuweka saa mbele ya kioo, always on display pamoja na vinpengele vingine vidogo vidogo.

Advertisement

Toleo hilo jipya maalum kwa simu za Samsung Galaxy S 7 na S 7 Edge limepanga kuleta sehemu tu ya vipengele vilivyokwepo kwenye simu za Note 7 na sio Programu nzima ya simu hiyo. Hata hivyo bado hakuna taarifa zozote kuwa toleo hilo jipya litasambaa kote duniani hivyo kama bado hujapata toleo hilo usiwe na wasiwasi kwani Samsung bado hawaja tangaza kuwa toleo hilo litakua international.

Ili kuendelea kujua Samsung watafanya nini kipya kuwafuraisha zaidi wateja wake endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use