Taarifa za mtandao wa vine kufungwa sasa zimefikia kwenye hatua za mwisho, hivi karibuni kampuni hiyo ilitoa taarifa kwa watumiaji wake kuwa mtandao huo utasitishwa na kubadilishwa kuwa Vine Camera.
Katika taarifa hiyo iliyo andikwa kuwa programu za mtandao wa Vine zitaendelea kuwepo kwenye masoko yote ya Android na iOS lakini programu hizo zitabadilishwa kabisa na kuwa Vine Camera, ambapo mtumiaji atakuwa na uwezo wa kuendelea kutengeneza video sekunde 60 lakini mtumiaji atakuwa anapost kwenye mitandao mingine kama Twitter au hata kuifadhi video hizo kwenye simu yake.
Kwa sasa vine inaruhusu watumiaji wake kudownload video zake ambazo ziko kwenye mtandao huo,hii inatakiwa kufanyika kabla ya mtandao huo kubadilishwa. Vilevile mtandao huo utaamisha follower wote kutoka kwenye mtandao huo kwenda mtandao wa Twitter, hapo kutakuwa na meseji maalumu ambayo itakuwa ikiwauliza watu walio kufullow kama wanataka kukufuata kwenye mtandao wa Twitter, hata hivyo mtandao huo unategemea kubadilishwa ifikapo mwezi January mwaka 2017.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.