Vigezo hivi na mashari vimewekwa kwaajili ya kutoa muongozo jinsi ya kutumia ikiwa pamoja na kudhibiti utumiaji wa group la WhatsApp la Tanzania tech. Kwa kukubali kujiunga na Group hili unakubali kuwa utafutat vigezo na mashari haya.
- Hairuhusiwi kujiunga na Group hili kama una UMRI CHINI YA MIAKA 18.
- Hauruhusiwi kuanzisha au kuchangia mijadala isiyohusu maswala ya teknolojia
- Haurisiwi kutuma picha za matangazo ya biashara au link za matangazo yoyote ya biashara ndani ya Group.
- Haurisiwi kutuma nyaraka zako za siri kama password (nywila) email na vingine ambavyo vina aminika kuwa ni vya siri.
- Hauruhusiwi kuanzisha au kuchangia mijadala yoyote ambayo inavunja sheria za nchi ikiwa pamoja na sheria za makosa ya mtandao kwa ujumla.
- Hurisiwi kuanzisha au kuchangia kwenye mijadala yoyote yenye lengo la kumkashfu mtu watu au kampuni yoyote, kumtukana mtu watu au kampuni yoyote au kumkosea heshima mtu watu au kampuni yoyote.
- Hairusiwi kutuma picha zozote zisizo na maadili au zilizo nje ya mada kwa ujumla (nje ya mada ya teknolojia).
- Hurisiwi kuvunja sheria zozote zile zilizo wekwa na Group hili au mafanyakazi yeyote wa Tanzania Tech.
MUHIMU
- KUMBUKA kuvunja sheria hizi kunaweza kufanya wewe kuondolewa kwenye Group au kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na sheria ya nchi au mahali ulipo.
- NI MUHIMU kuzingatia kuwa sio kila mada ni lazima uchangie unaweza kuacha mada nyingine ambazo hazina umuhimu kwako.
- NI MUHIMU kuzingatia kuwa Group hili ni kwaajili ya kusaidiana au kupeana msaada wa kiteknolojia na sio vinginevyo.
- NI MUHIMU kutembelea ukurasa huu kila mara ili kuweza kujua mabadiliko haya ya vigezo na mashari ya utumiaji.
Vigezo na Masharti haya Vimeanza Kutumika Rasmi Tarehe 23-4-2018