Marekani imeweka historia mwaka huu kwa kuruhusu kulima na kutumia mmea wa bangi ambao wengi nchini humo hutumia mmea huo kama dawa. Kati hali hiyo kumeanza kutokea teknolojia mbalimbali ambazo zinasaidia wananchi hao wa marekani kulima bangi hiyo kwa urahisi.
Katika hali ya mshangao kampuni moja ya nchini marekani ilitengeneza kifaa kinacho kwenda kwa jina la Leaf, kifaa hichi kilichotengenezwa kwa mfano wa friji kinauwezo wa kutunza bangi kuanzia mbegu mpaka kuwa mmea kamili na hata katika zoezi zima la kukausha bangi hiyo.
Kifaa hicho hutumia kemikali maalum ili kuhakikisha bangi hiyo inakuwa kwenye mazingira bora na yenye hewa na kemikali zinazotakiwa. Pia Leaf huja na programu maalumu ya Android na iOS ambayo itakusaidia kuangalia maendeleo ya bangi yako inapokua ndani ya kifaa hicho.
Kifaa hicho kitauzwa kwa nchi za marekani na canada pekee kikiwa na bei ya dollar za marekani $2,990 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 6,600,000. Hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa bangi ni dawa za kulevya hivyo sidhani kama ni kitu cha msingi kuwa na teknolojia kama hizi duniani na hata hapa kwetu Tanzania.
Unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kwa kupata habari za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.