Wote tunajua kuwa programu ya VLC inakuwezesha kucheza video zenye format karibia zote, pia vile vile programu hii inakuwezesha kuangalia video za mtandao wa Youtube pamoja na hata kudownload video hizo. Lakini kama haitoshi hivi karibuni programu hiyo ya VLC imeongezewa lingine tena kwa kuwekewa uwezo wa kuonyesha video za nyuzi 360.
Kampuni yenye programu hiyo ya VLC VideoLan imeungana na kampuni ya utengenezaji wa kamera za nyuzi 360 (VR) maarufu kama Giroptic ili kufanikisha kuweka uwezo huo kwenye programu hiyo ya VLC. Kwa sasa unaweza kudownload programu ya majaribio yenye uwezo wa kuonyesha video za nyuzi 360 inayopatikana kwenye tovuti ya VideoLAN.
Kwa sasa programu hiyo inapatikana kwenye mifumo ya Windows na Mac pekee, lakini kampuni ya Video LAN imepanga kuleta programu hiyo kwenye mifumo yote ikiwemo mifumo ya Android pamoja na iOS.
Je nini maoni yako kuhusu ili tuandikie maoni yako hapo chini au pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.