Kwa mara nyingine ubora wa simu pamoja na toleo jipya la iOS 10 vyote vimeingia kwenye maswali wiki hii baada ya kugundulika kwa bugs ambao wanaweza kufanya simu yako kuganda (freeze) kwa muda baada ya ku-play video fupi ya sekunde tano.
Video hiyo iliyogunduliwa kwenye mtandao wa Reddit imethibitishwa kuadhiri simu za iphone zenye mfumo mpya wa iOS 10.1 na iOS 10.2 zote ziliganda baada ya ku-play video hiyo kwenye simu hizo, katika video iliyosambaa ilionyesha video hiyo ikitumwa kama link kwa njia ya iMassage baada ya kubofya link hiyo video hiyo huonekana kama vile imevunjika (Corrupt) hivyo huonekana ikicheza kwa kurudia rudia. Kisha baada ya hapo simu yako itaendelea kuwa kama kawaida na ndani ya sekunde tano au kumi utaanza kuona simu yako iki-anza kuwa slow na baadae kuganda kabisa.
Njia pekee ya kutoa simu yako katika kuganda huko ni kubofya kwa pamoja kibonyezo cha kuwasha pamoja na home (kibonyezo cha katikati) kwa muda baada ya hapo utaona simu yako ikirudia kwenye hali yake ya kawaida. Kama unataka kujaribu video hiyo kwenye simu yako ya iphone hii ndio link ya video hiyo https://vk.com/doc106491973_439166823 kumbuka kuwa makini usije kuharibu simu yako na usipokee video link yoyote kwenye simu yako kwa sasa mpaka Apple watakapo rekebisha tatizo hili, pia video hii ikiwa kwenye mfumo wa MP4 haina tatizo lolote hivyo ni lazima itumwe kama link.
Kama unataka habari za teknolojia kila siku endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.