Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Utaweza kutumia video yoyote bila kupata tatizo la Copyright kupitia YouTube
Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Ukweli ni kwamba kwa sasa video ni kila kitu ndio maana kwa sasa karibia kila kampuni inayo channel ya mtandao wa YouTube. Lakini pamoja na hayo ni ukweli usio pingika kuwa sio rahisi hata kidogo kutengeneza video bora ambayo itashindana na mamilioni ya video zinazo pakiwa kila siku kwenye mtandao huo.

Lakini, Je unajua kuwa ipo mitandao ambayo inakupa uwezo wa kupakua video za bure kabisa ambazo unaweza kutumia kwenye mtandao wa YouTube bila kuwekewa vikwazo vya Copyright.?

Advertisement

Kama ulikuwa hujui basi kupitia makala hii nitaenda kuonyesha mitandao mbalimbali ambayo itaenda kukusaidia kupata video hizo bure kabisa. Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Pixabay

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Pixabay ni moja kati ya mitandao ya siku nyingi na inayo aminika zaidi kwenye kutoa video za bure kwa ajili ya kutumia kwenye mitandao mbalimbali. Tovuti hii haikupi video tu, bali pia unaweza kupata picha ambazo unaweza pia kuzitumia bure kabisa kwenye video au sehemu yoyote ili bila kusumbuliwa kabisa na maswala ya copyright.

Tembelea Pixabay Hapa

Pexels

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Tovuti nyingine ni Pexels, tovuti hii inafanana kabisa na tovuti iliyopita na yenye pia inakuja na video mbalimbali ikiwa pamoja na picha ambazo unaweza kutumia kwenye mitandao yako ya kijamii kama YouTube bila kupata tatizo la Copyright. Unaweza kutembelea tovuti hiyo hapo chini.

Tembelea Pexels Hapa

Coverr

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Coverr ni tovuti nyingine ambayo inaweza kukusaidia sana kuweza kupata video za bure za kutumia kwenye mtandao wa YouTube, tovuti hii nayo haina tofauti sana na tovuti iliyopita, bali hii yenyewe inakuja na uwezo wa kupakua video pekee. Tovuti hii inakuja na video nyingi sana na uhakika utapa clip yoyote ile unayotaka kutumia kwenye video zako.

Tembelea Coverr Hapa

Videvo

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Videvo ni tovuti nyingine bora ya kusaidia kupata video za bure kwa asilimia 100, tovuti hii ni tofauti na tovuti nyingine kwenye list hii kwa sababu videvo inakusaidia kupata video pamoja na nyimbo ikiwa na sound effect mbalimbali ambazo unaweza kutumia kwenye video zako bila kupata tatizo la copyright. Tovuti hii inakuja na video nyingi sana zenye resolution ya 4K.

Tembelea Videvo Hapa

Mazwai

Tovuti za Kudownload Video za Bure za Kutumia YouTube

Mazwai ni tovuti nyingine na ya mwisho kwenye list hii, tovuti hii inakuja na mkusanyiko wa video mbalimbali ambazo unaweza kutumia ndani ya video zako ya YouTube. Kama ulikua unatafuta video bora za kutumia bila kupata tatizo la copyright kwenye video zako basi tumia tovuti hii ya mazwai kupata video fupi za kuchanganya kwenye video yako.

Tembelea Mazwai Hapa

Na hizo ndio website ambazo unaweza kuzitumia kupata video za bure kabisa kwaajili ya kutengeneza video yako bora. Baada ya kudownload video hizi unaweza kuzi unganisha na kuwa video moja kwa kutumia njia hii ya kutengeneza video za kuweka kwenye mitandao ya kijamii bila ujuzi. Njia hii ni bora sana na itakusaidia sana kutengeneza video bora.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use