Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Video: Afanyiwa Upasuaji wa Kichwa Huku Akipiga Gitaa

Sayansi imevuka mipaka na sasa upasuaji unafanywa hivi
Upasuaji Upasuaji
PICHA NA CNN

Katika Hospitali moja huko nchini India madaktari wame fanikiwa kufanya upasuaji wa aina yake na wakwanza kutokea kwenye historia ya Sayansi na Teknolojia. Mtu mmoja ambaye alikua na ugonjwa wa mishipa ya ubongo alifanyiwa upasuaji wa kichwa huku akiwa yupo macho tena huku anapiga gitaa.

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Abishek Prasad mwenye umri wa miaka 35 ni mtaalamu wa tehama na mwanamuziki na vilevile ni mtaalamu wa kupiga gitaa, Katika upasuaji huo uliotumia zaidi ya masaa 7 Prasad alionekana akiwa burudisha madaktari wake kwa kupiga gitaa lake kama mtu ambaye alikua hafanyiwi upasuaji wowote…

Advertisement

Hata hivyo madaktari walisema kuwa Prasad aligunduliwa na ugonjwa ambao unaweza kuonekana pekee pale atakapo cheza gitaa na ndio sababu ilibidi afanyiwe upasuaji huo huku akicheza gitaa.

Prasad kwa sasa amepona ugonjwa huo baada ya upasuaji huo kufanikiwa na amepanga kuacha kazi aliyokuwa anafanya mwanzoni kama mtaalamu wa tehama na sasa anataka kuwa mwanamuziki wa kisasa anaetumia gitaa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : CNN

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use