Thibitisha Akaunti ya Paypal Kupitia M-Pesa au Airtel Money

Utaweza kuongeza uwezo wa akaunti yako kupokea pesa zaidi
Thibitisha Akaunti ya Paypal Kupitia M-Pesa au Airtel Money Thibitisha Akaunti ya Paypal Kupitia M-Pesa au Airtel Money

Kama wewe ni mtu yoyote ambaye unafanya biashara au una nunua bidhaa mtandaoni basi ni lazima unafahamu Paypal. Kama ufahamu kuhusu Paypal basi unaweza kusoma makala yetu hapa kujua zaidi kuhusu Paypal.

Sasa mbali ya kuwa Paypal kwa hapa Tanzania haina njia rasmi ya kutoa pesa kwenda kwenye akaunti yako ya benki, lakini ni wazi kuwa unao uwezo wa kutumia Paypal kupokea pesa kutoka kwa mtu yoyote binafsi aliyopo nje ya nchi au kutoka kwa mtu mwenye akaunti ya Paypal.

Advertisement

Mbali ya kukosa uwezo wa kutoa pesa, unaweza kutumia Paypal kufanya malipo kwenye mitandao mbalimbali inayopokea pesa kupitia Paypal. Hivyo basi kama umetumiwa pesa na huwezi kutoa unaweza kutumia salio lako kufanya manunuzi kwenye mitandao mbalimbali na baadae kitu hicho kikifika nchini unaweza kukiuza na kupata pesa yako..

Verify Paypal kwa Mpesa na Airtel Money

Sasa ili kuongeza uwezo wa akaunti yako ya Paypal kupokea pesa zaidi ya kiwango cha chini kilicho wekwa ni lazima kuverify akaunti yako.

Kitu kizuri ni kuwa, Vodacom Tanzania na Airtel zina kuja na huduma ya Mastercard, Kupitia huduma hizi unaweza kuthibitisha akaunti yako ya Paypal na kuanza kupokea malipo kwa haraka kwa kutumia akaunti yako ya Paypal.

Sasa ili kuthibitisha akaunti yako unaweza kufanya hatua hizi rahisi kwa kutumia huduma ya mtandao mmoja wapo kati ya (Vodacom) M-Pesa Mastercard, au Airtel Mastercard.

Hatua ya kwanza ingia kwenye akaunti yako ya Paypal kisha bofya sehemu ya wallet, kama umeweka kadi bofya kadi unayotaka kuverify, kama hujaweka kadi bofya sehemu ya Link card na link kadi yako kwanza kwenye akaunti yako ya Paypal.

Thibitisha Akaunti ya Paypal Kupitia M-Pesa au Airtel Money

Baada ya ku-link card ya benki, moja kwa moja utaweza kupata sehemu ya Confirm. Kumbuka unaweza usione mara moja sehemu ya kuverifiy, hivyo hakikisha una angalia zaidi sehemu ya wallet kadri siku zinapo enda.

Sasa baada ya kubofya sehemu ya Confim au verify, moja kwa moja utakatwa gharama kama TZS 2400 hivi na moja kwa moja utapewa code ambazo unatakiwa kujaza kwenye akaunti yako mara baada ya kubofya sehemu ya verify au confirm.

Sasa code hizi zinapatikana kwenye meseji ambayo unatumiwa na Vodacom M-pesa Mastercard, meseji hii inakuwa na namba ambazo zipo nne na unatakiwa kuandika namba hizo kwenye sehemu iliyopo wazi kwenye ukurasa wa ku-verify.

Thibitisha Akaunti ya Paypal Kupitia M-Pesa au Airtel Money

Kama unavyoweza kuona meseji inaweza kuwa kama hii, kitu cha msingi ni namba ambazo unaziona baada ya neno Paypal. Unacho takiwa kufanya ni kunakili au kucopy namba nne za mwisho na kuziandika kwenye ukurasa wa verify kisha bofya Verify.

Baada ya hatua hizo moja kwa moja utakuwa umethibitisha akaunti yako na utaweza kupokea pesa zaidi na utaweza kufanya manunuzi kwa urahisi na haraka. Kama unafikiria kutoa pesa kwenye akaunti yako ya paypal unaweza kujaribu njia hii hapa.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania tech nakuahidi hutojutia kujiunga nasi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use