Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Haya hapa yote ambayo utegemee kuyaona kwenye uzinduzi wa iPhone 14
Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14 Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Tukio kubwa zaidi la mwaka la Apple na uzinduzi wa iPhone 14 hatimaye limetufikia. Tukio hilo ambalo limepewa jina la ‘Far Out’ linafanyika huko nchini marekani kwenye makao makuu ya kampuni ya Apple maarufu kama Apple Park.

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Advertisement

Kupitia mkutano huo ambao unafanyika leo kuanzia 20:00 PM saa mbili ya usiku kwa muda wa saa za afrika mashariki, yafuatayo ndio mambo ambayo pengine utegemee kuyaona leo kwenye mkutano huo.

Uzinduzi wa iPhone 14

Hili ni tukio kuu la Apple na kutokana na desturi ya Apple tukio lote litakuwa ni kwaajili ya iPhones mpya. Kwa mujibu wa ripoti Apple itazindua simu nne mpya za iPhone 14 – iPhone 14 ya inchi 6.1, iPhone 14 Pro na iPhone 14 Plus ya inchi 6.7 na iPhone 14 Pro Max.

Hata hivyo inasemekana kuwa Apple imerudi kwenye toleo la simu ya bei nafuu zaidi ya ukubwa wa Plus kutokana na kuwa, gharama ya iPhone mini inachukuliwa kuwa ghali na pia hatua hii inakuja kutokana na mauzo ya kukatisha tamaa yaliyotokea kwenye toleo.

Muonekano iPhone 14

Hata hivyo kwa mujibu wa tetesi zaidi, IPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max zitapata sehemu mpya ya ukingo wa juu (Notch) ambapo sehemu hiyo sasa itakuwa imekatwa na kamera za selfie na FaceID, zitaunganishwa ndani ya sehemu hiyo ya notch, hata hivyo sehemu hiyo pia itatumika kuonyeshea viashiria vya faragha kama kipaza sauti na kamera zinapokuwa zinatumika.

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Kamera za iPhone 14

Kamera kuu itakuwa na uwezo mpya wa hadi Megapixel 48 ambayo itawezesha kurekodi video za hadi 8K. Kamera ya selfie hatimaye itapata teknolojia ya AF autofocus, pia kutakuwa na maboresho mbalimbali kwenye kamera hizo.

Hata hivyo tetesi zinasema kuwa iPhone 14 Pro itapata aina mpya ya chipset ya A16 Bionic ambayo inasemekana kuwa na nguvu zaidi.

Kwa matoleo ya iPhone 14 ambazo sio toleo la Pro, Zitaendelea kutumia A15 Bionic ya mwaka jana na kuna uwezekano mkubwa kuwa matoleo hayo yatarithi kamera pana kutoka kwa iPhone 13 Pro. Baadhi ya fununu zina onyesha kuwa matoleo hayo yatapata kamera iliyoboreshwa, lakini ripoti hazina uhakika kuhusu uwezekano wa AF (Auto Focus) kwenye kamera za selfie kwa matoleo hayo.

iPhone mpya zitaendelea kutumia USB ya Lightning port kwa mwaka mwingine, lakini zinaweza kuongezewa kasi ya kuchaji hadi 30W.

Bei ya iPhone 14

Aina za Pro huenda zikaongezeka bei kwa hadi TZS 300,000 zaidi kwa nchini na kwa takribani $100 kwa nchi za Marekani na Ulaya.

Aina zote za iPhone 14 zinaweza kuwa na usaidizi mpya wa ubunifu na muunganisho wa satelaiti, ambao Apple ilijaribu kuzindua mwaka jana lakini haikuweza kukamilika. Kampuni ya Satellite Globalstar imehusishwa na kutoa baadhi ya huduma za Satellite zitakazo unganishwa na simu hizo.

Uzinduzi wa Watch Series 8, Watch Pro, Watch SE

Uzinduzi mwingine baada ya iPhone itakuwa ni uzinduzi wa saa janja za Apple Watch, kwa mujibu wa tetesi tegemea kuona Apple Watch Series 8.

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Tarajia kuona saa hizo zikipata aina mpya ya chipset ya S8 yenye kasi zaidi. Pia kuna uwezekano wa kuona saa hizo zikiwa na aina mpya ya sensor yenye kudhibiti na kugundua halijoto ya mwili na kuweza kumpa taarifa mtumiaji aliyevaa saa hiyo kama amepata dalili za homa.

Toleo Jipya la Watch Pro

Hata hivyo Apple inatarajiwa kutoa saa mpya ya Watch Pro, ambayo itakuwa kubwa 47mm – kutoka saizi ya 41mm na 45mm ya saa zilizo zoeleka sasa za Apple. Tetesi zina pendekeza Watch Pro inaweza kuwa na muonekano tofauti kidogo na bei yake inatarajiwa kuwa kati ya $900-$1000.

Mbali na hayo pia kutakuwa na toleo jipya la Watch SE ambalo pia litakuwa na chip mpya ya S8 chip, lakini muonekano pamoja na ukubwa wa kioo utakuwa ule ule.

Uzinduzi wa AirPods Pro 2 and iOS 16

Kwa upande wa AirPods Pro za miaka mitatu iliyopita sasa zinapata mbadala kwani kutokuwa na toleo jipya la AirPods Pro mpya ambazo zitakuwa zinatumia teknolojia mpya ya Apple’s Lossless Audio Codec (ALAC), ambayo inawezesha matumizi bora zaidi ya Bluetooth.

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Mbali na hayo yote simu zote za iPhone 14 zinategemewa kutumia mfumo mpya wa iOS 16 ambao unakuja na maboresho mengi sana, Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma makala hapa.

Na hayo ndio yote ambayo unaweza kutegemea kuyaona kwenye uzinduzi wa iPhone 14, kama unataka kufuatilia mubashara uzinduzi huo tutakuwa LIVE moja kwa moja kupitia Tanzania Tech tukikuletea yote yatakayo jiri kwenye uzinduzi huo.

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia unaweza kupakua app ya Tanzania Tech kupitia Play Store kupata habari moja kwa moja.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use