Kampuni maarufu ya teknolojia ya nchini marekani ya Google hivi karibuni imeanza kutuma mialiko kwa watu mbalimbali kuwakaribisha katika tamasha litakalo fanyika mwezi October ambapo kampuni hiyo ya Google inatarajia kutangaza simu yake mpya ya Pixel pamoja na Pixel XL.
Hata hivyo tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 4 huko mjini San Francisco ambapo simu hizo mpya zitabatizwa rasmi kutoka jina la Nexus na kuwa Google Pixel, taarifa kutoka vyazo mbalimbali zinasema kuwa simu hizo mpya zitakua na kioo cha Inch 5 kwa Google Pixel pamoja na kioo cha inch 5.5 kwa Google Pixel XL .
Bado haijajulikana kama Google watazindua simu hizo Pekee au watakuja na kitu kingine kipya, ili kujua haya na mengine mengi jiunge nasi hapa Tanzania tech kwani tutakua tukionyesha live tamasha zima la uzinduzi huo utakao fanyika katika mji wa San Francisco huko nchini marekani.
Ili kuhakikisha kuwa hupitwi na tamasha hilo pamoja na habari zote za teknolojia hakikisha unatembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.