Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Tumia tovuti hizi kurahisisha kazi ambazo unafanya kupitia progamu mbalimbali
Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake
©99designs.com

Ni wazi kuwa programu mbalimbali ni msingi wa mwana teknolojia yoyote, lakini ni wazi kuwa zipo njia kadhaa ambazo unaweza kuepuka kupakua programu nyingi kwenye kompyuta au simu yako na badala yake utaweza kutumia tovuti ambazo kwa namna moja ama nyingine hufanya kazi sawa na programu husika.

Kupitia makala ya leo tutaenda kuangalia tovuti ambazo zitaenda kusaidia kufanya mambo mbalimbali ambayo hufanywa na programu ambazo ni lazima ku-install kwenye kompyuta au simu yako. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Advertisement

Tumia Photopea Kama Photoshop

Kama wewe ni mtumiaji wa programu ya Adobe Photoshop basi huna haja ya kutumia programu hii kila mara kwani sasa unaweza kutumia tovuti ya Photopea ku-edit picha zako kama kwenye programu ya Photoshop.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Kama unavyoweza kuona kwenye picha utaweza kufanya kazi kupitia layers na kila kitu kilichopo kwenye programu ya Photoshop utakikuta kwenye tovuti hii. Unaweza kutembelea tovuti hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Tumia InVideo Kuedit Video

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao mara nyingi hufanya kazi ya kuedit video basi huna haja ya kupakua programu nyingi kwenye kompyuta yako, tena hasa kama unataka kufanya kazi ya kuedit video za kawaida. Tovuti ya InVideo inakupa uwezo wa kuedit video bora sana kwaajili ya kuweka kwenye mitando ya kijamii.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Kizuri ni kuwa, tovuti ya invideo inakuja na mifano au templates ambazo unaweza kutumia kuedit video zako kwa haraka na urahisi. Unaweza kujaribu tovuti hii kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Tumia VirusTotal Kama Antivirus

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unapokea mafaili mbalimbali mara kwa mara kwenye kompyuta yako, basi ni wazi kuwa unahitaji programu ya Antivirus. Lakini pia, unajua kuwa unaweza kutumia tovuti ya VirusTotal kuweza kujua kama mafaili unayo pokea ni salama ?.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Kupitia VirusTotal unaweza ku-scan link mbalimbali ikiwa pamoja na mafaili mbalimbali. Tovuti hii imekuwa ni msaada mkubwa kwangu binafsi kwa kuwa naitumia mara zote napotaka kupakua programu kutoka kwenye tovuti fulani. Unaweza kujaribu VirusTotal kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Tumia Figma Kutengeneza Logo na UIX

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao ni frontend developer, na mara nyingi umekuwa ukitengeneza prototype au logo kwaajili ya wateja wako basi Figma ni tovuti bora kwaajili yako. Figma ni tovuti ambayo inalinganishwa na programu ya sketch ya mfumo wa MacOS.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Kupitia tovuti hii ya Figma utawza kutengeneza Logo pamoja na prototype mbalimbali kwa urahisi huku ukiwa na uwezo wa kushare na timu yako kwa urahisi. Unaweza kujaribu tovuti ya Figma kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Tumia PDF Escape Kuedit PDF

Tulisha wahi kuongelea jinsi ya kuedit PDF, lakini kama umesoma makala hiyo ni wazi kuwa unajua kuwa ni lazima kutumia programu fulani. Lakini sasa huna haja ya kutumia programu kama Adobe PDF kwani tovuti ya PDF Escape itakusaidia kuedit PDF kwa urahisi na haraka.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Tovuti hii ni bora sana kwa wale ambao wanatumia PDF mara nyingi kwa siku, kizuri ni kuwa tovuti hii ni bure kutumia na unaweza kutumia bure bila kuwa na haja ya kulipia kwa matumizi ya kawaida. Unaweza kujaribu tovuti hii kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Tumia Small PDF Kubadilisha PDF

Kwa kuwa tumeongelea PDF basi tumalizie list hii kwa tovuti ya Small PDF, tovuti hii itakupa uwezo wa kuconvert PDF kwenda kwenye format yoyote. Mbali na hayo utaweza kufanya mambo mengi sana yanayohusu PDF.

Usipakue Programu Hizi, Tumia Tovuti Hizi Badala Yake

Tovuti hii ni bora pengine kuliko programu yoyote ya PDF kwani utaweza kufanya mambo yote unayo hitaji kwenye PDF bila ku-install programu yoyote kwenye kompyuta au simu yako. Jaribu Tovuti hii kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Na hizo ndio tovuti ambazo unaweza kuzitumia badala ya programu mbalimbali, kumbuka tovuti nyingi kwenye list hii ni bure kabisa kutumia na nyingine utaweza kutumia bure kwa muda maalum au kwa viwango maalum.

Kama unata kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua tovuti bora ambazo unaweza kuzitumia kujifunza kutengeneza tovuti na apps mbalimbali kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi na makala kama hizi, hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use