Kwa sasa nadhani karibia Tanzania nzima wananchi wote wanatumia Luku kupima kiwango cha matumizi ya umeme wa kila siku, Matumizi haya ya Luku yamebadilisha kabisa jinsi tulivyokuwa tunatumia umeme hapo awali kwa maneno mengine ni kwamba kwa sasa watu wengi wanaonekana kutumia umeme kwa ustaarabu mkubwa kuliko hapo awali kwani mfumo huu wa Luku umeleta mipango ya kutumia kadri unavyo nunua na nunua kadri unavyotumia.
Mipango hii ndio inyofanya leo niandike makala hii kwani watu wengi sana wanao kaa kwenye nyumba za kupanga ndio wanaoadhirika sana na mipango hiyo. kwa mfano kuna wakati unakuta labda wewe huna kitu ndani kwako lakini pesa unayoambiwa uchangie pengine ni kubwa kuliko matumizi yako hivyo unakuta mfumo wa kulipia kadri unavyotumia unakuadhiri moja kwa moja. Lakini kama haitoshi pengine wewe ni mtu ambaye ushindi nyumbani hivyo unakuta hela unayotoa kununua umeme haifikishwi yote na unakuta umeme unao-wekwa ni mdogo kuliko dhamani ya pesa yako uliyo toa hivyo unakuta unalipa zaidi ya unavyotumia na pengine pesa uliyotoa kununua umeme huo si sawa na kiwango cha unit kilichowekwa.
Basi kama wewe ni mmoja wa watu hao endelea kusoma makala hii kwani mpaka mwisho wa makala hii utaweza kujua namna ya kuangalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku ikiwa ni moja kwa moja kwenye mita yako hiyo. Kwa kuanza basi nadhani kila mtu atakua anaijua mita ya Luku jinsi ilivyo pamoja na muonekano wake pale unapo ingiza tarakimu ili kuweka umeme, pia najua mita zinatofautiana lakini naimani njia hii inafanya kazi karibia kwa kila mita za Luku ambazo zinatumia vibonyezo vya namba.
Basi kama mita yako iko hivyo moja kwa moja ili kuangalia kiwango cha umeme kwenye mita yako hakikisha kuna umeme kisha bofya namba 2 pamoja na kibonyezo cha kuweka umeme (Enter) hakikisha unabonyeza vyote kwa pamoja kisha achia.
Baada ya hapo utaona namba za kwanza ambazo ndizo zinaonyesha kiwango cha umeme kilicho wekwa kwa mara ya mwisho kwenye mita yako ya Luku, hakikisha unaangalia namba za kwanza zinazo anza kutokea kwenye kioo cha mita yako kwani namba hizo hubadilika na baadae baada ya kama sikunde 3 namba hizo hurudia hali yake ya awali na kuendelea kuhesabu kiwango cha umeme uliopo hivyo kama utakua ujaona vizuri basi subiria namba hizo zirudi kwenye hali yake alafu urudie tena kufanya hatua hizo.
Angalizo : Njia hii ni salama kabisa lakini kumbuka Mita ya Luku ni mali ya Tanesco hivyo ni vyema kufanya hatua hizi kwa uangalifu usije kuharibu au kubadili chochote kwenye mfumo wa mita yako.
Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kungalia kiwango cha mwisho kilichowekwa kwenye mita yako ya Luku kama una maswali unaweza kuuliza kupita hapa kama una maoni au ushauri unaweza kutuandikiwa hapo chini na ili kupata habari zote za teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.
Maoni*nnimejaribu kufanya hivyo mbona mita ya kuchomeka imeziima kabisa haiwaki ?
nimejaribu kufanya hivyo mbona mita ya kuchomeka imeziima kabisa haiwaki tena?
Kwani umefanyaje mita yako.
Na hii ni maalum kwenye mita unazo ona hapo kwenye picha.
Maoni* Maoni Yangu ni kwamba kama imewezekana kuweka unit za luku kwa njia ya simu basi hata kuangalia kiwango cha unit iliyopo kwa cm inawezekana… iwekwe hiyo system ili hata ukiwa mbali na meter unaweza kuangalia na kuweka kama Salio kwenye cm asanten sana
Naomba kujua utaratibu au fomula ya namna ya kuhamisha token kutoka mita moja kwenda nyingine kama umekosea mita namba.
Naomba kujua fomular ya kurudisha/ kuhamisha token toka mita namba moja kwenda mita namba nyingine kama umekosea namba ya mita.
Tafadhali tembelea ofisi za Tanesco ili kujua hilo.
Nilivyotumia r/,control KWA kubonyeza number 2 ikiambatanisha Na enter majibu nayapata 77 Na kuonesha error kwann
Naomba kuuliza kwa kiwango kidogo cha umeme yan umeme wa nyumbani unatakiwa ukinunua uczid sh ngap kwa mwezi na mwez ni siku ngapi? coz mwez wa pil una cku 28
naomba nmiangalizie Mara ya mwisho umeme umewekwa wa shilingi ngapi,na nlipata units ngapi? kwenye
meter no.24214532459
bei ya mita ya umeme ni Tsh ngapi?
Mita yangu ilitolewa service charge mwezi january ila kwa sasa imerudishwa kula umeme kama vile nina kiwanda ndg nisaidiye nikiweka umeme wa elfu5 ni kama sijaweka chochote
Naweza pata statement ya malipo ya kila mwezi yanayo fanyika kwa meter yangu kwa njia ya mtandao?
Ndio lakini utaweza kuona idadi ya mwisho kwa mwezi husika tu! kupitia app ya GEPG ambayo unaweza kudownload kupitia Play Store. Ukitaka taarifa zaidi unaweza kwenda kwenye kituo cha huduma kwa wateja cha Tanesco.
mbona sisi tupo wapangaji wawili na tumefungiwa hiyo submeter alaf tukaweka umeme wa elf10 tukapata unit 28 ila toka ifungwe mpaka sasa inasoma kila mmoja 116 na moja inasoma 114 ila kwenye mita ukiangalia token zimebak 4 sasa nashindwa kuelewa msaada wenu