Kuanzisha kitu hadi kiweze kufanikiwa sio kazi rahisi hata kidogo, lakini pia kufurahia mafanikio ya kitu hicho hasa pale unapo fanikiwa sana pia sio kazi rahisi hata kidogo. Haya yanajionyesha kwa mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa Facebook ambaye hutumia zaidi ya dollar za marekani $22.6 milion kwa mwaka ambayo ni takribani zaidi ya Tsh Bilioni 50 kwaajili ya ulinzi.
Ulinzi ninao zungumzia hapa ni ulinzi binafsi wa mwanzilishi huyo ikiwa pamoja na familia yake, inasemekana mwaka 2018 Zuckerberg hutembea na walinzi zaidi ya wanne ambao wote kwa pamoja hulipwa zaidi ya dollar za marekani $200,000 ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 400 kwa sasa.
Mark Zuckerberg ambaye kwa sasa anashikilia namba 8 katika list ya watu tajiri duniani, kwa sasa inasemekana inatumia zaidi ya dollar milioni $2.6 kwaajili ya usafiri wa binafsi wa ndege (private jets) usafiri ambao unasemekana ni sehemu ya ulinzi wake.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya theguardian, matumizi kwaajili ya ulinzi wa mwanzilishi huyo yameongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka juzi (2017) ambapo inasemekana alikuwa akitumia zaidi ya dollar za marekani milioni $4.26 ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 9.
Hata hivyo matumizi hayo ya zaidi ya Tsh bilioni 50 ni matumizi ya mwaka jana 2018 pekee na inawezekana matumizi hayo yataongezeka kwa mwaka 2019 kutokana na matatizo mbalimbali ya kampuni hiyo.
Tofauti na hayo unaweza kusoma hapa kujua mambo mengine ambayo inawezekana ulikuwa hujui kuhusu Mark Zuckerberg na kampuni yake ya Facebook. Kwa makala zaidi za Je Wajua unaweza kusoma kipengele cha Je wajua.