Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ongeza Ukubwa wa Kioo cha Simu Yako kwa Kutumia Superscreen

Sasa unao uwezo wa kuongeza ukubwa wa simu yako kwa urahisi kwa kutumia kifaa hichi
Superscreen Superscreen

Kuna wakati unatamani kutumia simu yako kwenye screen kubwa, inawezekana unataka kucheza game au hata kusoma meseji zako za mitandao ya kijamii, sasa huna haja ya kuwa na wasiwasi tena kwani sasa kuna superscreen.

Kifaa hichi cha super screen kina uwezo wa kubadilisha screen ya simu yako kuwa screen kubwa zaidi, unachotakiwa kufanya ni kuinstall App maalumu ya superscreen kisha vitu vyako vyote vityanza kuonekana kupitia superscreen. Kifaa hichi kinakupa uwezo wa kufanya yote haya bila kuweka waya au bluetooth au waya au hata wireless yoyote ile.

Advertisement

Kifaa hichi kinauwezo wa kukaa umbali wa futi 100 kutoka simu yako huku kikiwa na uwezo wa kukaa na chaji zaidi ya masaa 12. Hivyo sasa huna haja ya kuwa na Tablet bali sasa utaweza tumia kifaa hichi cha superscreen ambacho kinauwezo wa kuamisha simu yako ya kawaida kwenda kwenye kifaa hicho cha superscreen chenye kioo cha ukubwa wa inch 10.

Supercreen ina kamera mbele na nyuma pia ina bluetooth, wireless pamoja na spika zenye kukupa uwezo wa kusikilza chochote kutoka kwenye simu yako. Kifaa hichi kinauzwa dollar za marekani $99 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 230,000. Kwa sasa kifaa hicho bado kiko kwenye hatua za mwisho ili kuingia sokoni na kinafaa kwenye mifumo yote ya Android na iOS, ili kujua superscreen itapatikana wapi endelea kutembelea Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use