Kampuni ya simu za mkononi Infinix hivi majuzi ilizindua Infinix HOT 30 kwa nchi za ugaibuni. Sasa, inajiandaa kuzindua Infinix HOT 30 nchini Tanzania.
Infinix kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz inahashiria ujio wa simu hiyo April 25.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali duniani kama GIZMOCHINA, KLGadgetTV na nyenginezo zimedai kuwa Infinix HOT 30 inaufanisi wa hali ya juu hivyo inaelezwa kuwa soko la simu za kima cha kati kuja kuwa hatarini.
Infinix HOT 30 imeudwa na kichakataji chenye misingi 8 cha MediaTek Helio G88 ikiwa na core mbili kali za ARM Cortex A75 na 2.0GHz, inahakikisha uchezaji laini wa games mitandaoni.
Kwa kuongeza, nguvu ya battery ya mAh5000 yenye kuhimili utumizi wa muda mrefu pasipo kuishiwa moto kiholela kunaipa hadhi HOT 30 kuwa simu bora zaidi duniani kote kwa mwenye kipato cha kati.
Infinix HOT 30 inasemekana kuwa na uwezo wa kuongeza ufanisi wa kumbukumbu/Memory kutoka Ram ya GB8 hadi 16GB ili kuwezesha uanzishaji wa haraka wa michezo/games na kufanya kazi nyingi kwa kasi ya hali ya juu, kama haitoshi pia inasadikika kioo cha HOT 30 ni smooth/laini zaidi wakati wa utumiaji kimeudwa na refreshrate 90Hz, touch rate 270 na teknolojia ya uboreshaji eneo la giza DRE inasemekana Infinix HOT 30 ni simu ya pekee kuwahi kuwepo kwenye series ya simu hizi.
Kuhusu bei na sifa nyengine za simu hii tembelea @infinixmobiletz mara kwa mara.