Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Soma hapa kabla ya kununua simu mpya ya Infinix S5
Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5 Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Hivi karibuni kampuni ya Infinix ilizindua simu mpya ya Infinix S5 hapa Tanzania, Simu hii ni moja kati ya simu bora za infinix na ambayo inapatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na uwezo wake. Mbali ya kuwa ni simu ya bei nafuu, simu hii pia inakuja na mambo mbalimbali ambayo huwenda kwa namna moja ama nyingine unaweza kuwa ulikuwa huyajui.

Kupitia makala hii nitaenda kukujuza baadhi ya mambo hayo ambayo yanaweza kufanywa na simu hii ya Infinix S5, ikiwa pamoja sifa na uwezo wa simu hii mpya. Basi bila kuendelea kupoteza muda, twende tukangalie mambo hayo.

Advertisement

Kupokea na Kukata Simu

Kama unakumbuka siku za karibuni tuliongelea jinsi ya kupokea au kukata simu bila kushika simu yako, kama unakumbuka njia hii ilikuwa ni lazima kutumia application. Sasa kupitia simu mpya ya Infinix S5 utaweza kupokea au kukata simu kwa njia ya kisasa bila kushika simu yako na bila kuongeza programu yoyote.

Kwa kutumia mkono wako unaweza kukata simu bila kuishika kabisa, kwa kuonyesha ishara ya mkono au Hi 5 ?? utaweza kukata simu na kwa kuonyesha alama ya Peace ✌? utaweza kupokea simu yako moja kwa moja bila kuishika. Sehemu hii inakupa msaada mkubwa sana kama mikono yako itakuwa imeshika kitu ambacho sio rafiki kwa simu yako na hutaki kuchafua simu yako. Unaweza kuwasha sehemu hii kupitia sehemu ya Settings > kisha tafuta Air Gestures.

Njia Mpya ya Kutumia WhatsApp

Mbali na ubora wa simu hii kwenye kamera, Infinix S5 imetengenezwa maalum kwaajili ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwa pamoja na WhatsApp, kupitia simu hii utaweza kutumia programu ya WhatsApp kwa namna ya kipekee ikiwa pamoja na kuhifadhi Status za WhatsApp za marafiki zako zaidi ya masaa 24 bila kutumia programu yoyote.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Unaweza kuchagua unataka status hizo zihifadhiwe kwa muda gani kuanzia siku 15 au kama unataka kubakinazo kwa muda zaidi ya miezi miwili pia unaweza kuchagua sehemu hiyo, Status za marafiki zako ambazo utakuwa umezingalia zitahifadhiwa kwenye simu yako moja kwa moja.

Mbali na hayo pia unaweza kutumia sehemu ya “Beauty Mode” kupitia WhatsApp Call, sehemu ambayo inaweza kufanya ngozi yako kuwa angavu pale unapo piga simu za video kupitia programu ya WhatsApp.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Unaweza kupata sehemu hizi na nyingine nyingi kupitia sehemu ya XOS Lab kupitia sehemu ya settings kisha chagua Social turbo.

Kamera ya Mbele

Kwenye simu hii mpya ya Infinix S5, kamera hii ya mbele ni moja kati ya kivutio kikubwa sana, ukiachana na kuwa kamera hii ipo juu ya kioo, infinix S5 inakuja na selfie yenye uwezo wa hadi Megapixel 32. Kamera hii ni bora sana kwa wapenzi wa selfie kwani inakupa njia mpya na za kisasa kabisa za kupiga picha zako.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Mbali na ubora wa kamera hii, Infinix S5 inakuja na njia za kisasa kabisa za kuonyesha kama unatumia kamera ya mbele, kwa mfano sehemu ya kamera ya mbele huwaka kuzunguka kamera pale unapo washa au unapotumia kamera ya mbele. Kamera hii pia inakuja na mfumo wa AI pamoja na HDR mfumo ambao hufanya picha zako kuwa angavu na zenye rangi bora zaidi.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Mbali na yote unaweza kutumia kamera ya mbele ya simu hii kuleta muonekano bora na wakisasa kwenye simu yako kwa kuweka wallpaper ambazo zitatumia sehemu ya kamera ya mbele kuweka muonekano mzuri sana kwenye simu yako. Unaweza kuwa mbunifu kwa kutafuta wallpaper bora zitakazo badilisha kabisa simu yako.. Trust me nimejaribu na ukweli inavutia sana.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Kamera za Nyuma

Kwa upande wa kamera za nyuma hapa sina haja ya kusema mengi sana kwani simu hii ni moja kati ya simu za Infinix zenye kamera bora hasa kama wewe ni mpenzi wa picha. Infinix S5 kwa nyuma inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 16, kamera nyingine zikiwa na Megapixel 2, Megapixel 5 pamoja na AI kamera (VGA Low light camera).

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Sasa kama wewe ni mpenzi wa kupiga picha hasa kwenye matukio utaipenda simu hii ya Infinix S5, simu hii ni bora hasa kipindi hiki cha sikukuu ambapo kunakua na mjumuiko wa familia ndugu na jamaa kwenye moment mbalimbali. Kamera ya Megapixel 16 ambayo ni wide lens hii ina uwezo mzuri sana wa kuchukua picha za kikundi cha watu na watu wote wakatoshea kwenye picha bila wewe kusogea mbali, yani hata kama eneo ulilopo ni dogo.

Kamera nyingine kwenye simu hizi ni bora pia kwani zitakupatia muonekano bora wa picha zako kwa kuangalia kiasi cha mwanga kutokana na eneo ulipo, huku mfumo wa AI ukisaidia kurekebisha rangi ili kusudi uweze kupata picha angavu zaidi zenye muonekano bora.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Kwa upande wa Video kamera hizi zinafanya vizuri sana hasa unapotumia kamera zote kuchukua video za 1080p, Unaweza kuchukua video bora zenye muonekano wa kisasa huku teknolojia ya AI ikisaidia kubadilisha mwanga kwenye video zako kulingana na eneo ulilopo, unaweza kuona mwenye uwezo wa simu hii kwenye kamera kwenye video fupi hapo chini.

Battery na Mengine

Upande wa battery simu hii inaweza kuimili kudumu na chaji kwa matumizi yote ya kawaida kwa mtumiaji yoyote wa simu ya Android. Unaweza kucheza game kwenye simu hii unaweza kuangalia video kwa muda zaidi ya lisaa bila chaji kupungua chini ya asilimia 90, pia unaweza kucheza game zenye uwezo mkubwa kama PUBG bila simu hii kuisha chaji kwa haraka, Unaweza kuangalia hapo chini kujua ninacho maanisha.

Kwa upande wa ubora simu hii inajua na ubora wa hali ya juu kwani inakuja na kioo kigumu kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya kuweza kuimili matumizi ya watu wote, pia vilevile ndani ya box la simu hii unapewa kava ambalo unaweza kutumia kulinda zaidi simu yako isipate michubuko pamoja na mikwaruzo hasa inapokuwa mfukoni kwako hasa kama umevaa nguo za kisasa zinazobada kidogo kwenye sehemu ya mifuko.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Kama hili mbali ya kulinda simu yako pia linafanya simu yako inakuwa na muonekano mzuri zaidi hasa kama hujazoea kutumia simu bila kava. Pia ukishika simu hii ikiwa na kava hili ina feel vizuri mkononi na sio rahisi kwa simu hii kuteleza pale inapokuwa na kava hili.

Teknolojia Ilivyoweza Kutumika Katika Toleo Jipya la Infinix S5

Hitimisho

Kwa ufupi kabisa kama unataka kununua simu kipindi hichi cha sikukuu basi hakikisha simu hii mpya ya infinix inakuwa kwenye list ya simu za infinix ambazo ungependa kununua. Simu hii kwa sasa inapatikana hapa Tanzania na unaweza kuipata kwenye maduka mbalimbali ya Infinix ikiwa pamoja na mawakala ambao wako nchi nzima.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use