Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Angalia Ubora na Ugumu wa Simu Mpya ya Huawei P20 Pro

Je simu ya Huawei P20 Pro inaubora gani kwenye matumizi ya kila siku..?
ubora na ugumu Huawei P20 Pro ubora na ugumu Huawei P20 Pro

Siku za nyuma kidogo Huawei ilizindua simu yake ya Huawei P20 pamoja na P20 Pro, simu hii ilikuja na ubora wa hali ya juu pamoja na aina mpya ya kamera kwa simu za Huawei. Kwa wale ambao mlisoma makala iliyopita kuhusu simu hii lazima utakuwa unajua nazungumzia nini, lakini pia kama ukusoma makala hiyo unaweza kusoma hapa.

Huawei P20 Pro ni simu ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya Huawei yenye kamera tatu, simu hii ukweli kabisa inakuja na muonekano mzuri sana pia kwa mujibu wa wachambuzi mbalimbali kamera tatu za simu hiyo zinachukua picha vizuri sana pengine kuliko hata simu mpya ya Galaxy S9 Plus. Pamoja na hayo je vipi kwenye ubora wa simu hii..?

Advertisement

Hapa utaweza kujua ubora wa simu hii kwa kuangalia simu hii ikipitia majaribio mbalimbali, kama vile majaribio ya kukwaruzika, majaribio ya kioo kupata joto pamoja na majaribio ya kukunjika. Bila kusahau unaweza kuangalia pia yaliyomo ndani ya simu hiyo, basi bila kupoteza muda twende tukangalie ubora wa simu hii ya Huawei P20 Pro.

Baada ya kuona ubora wa Huawei P20 Pro bado haija ishia hapa, unaweza kuendelea kuangalia yaliyomo ndani ya simu hii… yaani ni vifaa gani vilivyoko ndani ya simu hii vinavyofanya simu hii kuwa bora na je utaweza kubadilisha baadhi ya vitu ikitokea simu hii imeharibika..? Basi angalia hapa.

Mpaka hapo najua utakuwa umeshajua kama hii ni simu itakayo kufaa au laah, kama una moni yoyote au maswali unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini..

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use