Hatimaye Huduma ya Uber EATS Yaingia Rasmi Afrika Mashariki

Afrika mashariki kufurahia huduma mpya ya kuagiza chakula
Uber EATS Uber EATS

Hatimaye wapenzi wa kula chakula cha kuagiza hivi karibuni wataanza kufurahia huduma mpya ya kuletewa chakula kupitia huduma mpya ya Uber Eats. Kama ulikuwa huijui huduma hii ya Uber Eats ilianzishwa mwaka 2014 na kampuni ya Uber ambayo ni maarufu sana hapa Tanzania kwa kutoa huduma za usafiri binafsi kwa wakazi wa majiji mbalimbali ikiwa pamoja na Dar es salaam.

Huduma hii inaunganisha wateja na migahawa mbalimbali ili kuhakikisha unapata huduma ya chakula ukiwa sehemu yoyote ile. Huduma hii kwa sasa imeingia Afrika mashariki na kwa kuanza ita anzia nchini Kenya na huwenda baadae itakuja kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwa pamoja na Tanzania.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti ya Techweez ya nchini Kenya, Nairobi inakuwa ni moja kati ya miji minne pekee Afrika inayo hudumiwa na huduma ya Uber Eats miji mingine ikiwa ni pamoja na mji wa Cape Town, Johannesburg pamoja na Durban.

Kutumia huduma hiyo kama uko nchini Kenya unatakiwa kupakua App ya Uber Eats ya mfumo unao endana na simu yako Android au iOS au tembelea tovuti ya ubereats.com, kisha utaweza kuchagua mgahawa unaoupenda kisha utaweza kuagiza chakula unacho kipenda kutoka kwenye mgahawa huo. Vilevile kuna sehemu ya kutafuta ambayo, utaweza kutafuta chakula unacho kipenda au utaweza kutafuta mgahawa unao upenda ili kuagiza chakula kwa haraka zaidi.

Kwa sasa bado hakuna taarifa lini huduma hii itakuja Tanzania lakini bila shaka huduma hii itakuja Tanzania siku za karibuni na Tanzania Tech tutakuwa hapa kukupa taarifa zaidi kuhusu huduma hiyo mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use