Hivi karibuni mtandao wa Twitter umekuwa ukifanya maboresho mbalimbali ili kukidhi haja za watumiaji wake, Twitter ime-endelea kufanya hivyo hapo jana kwa kutangaza ujio wa sehemu mpya ya kuhifadhi tweet kwaajili ya kuisoma baadae.
Sehemu hiyo mpya ya Bookmark itakusaidia kuhifadhi tweet mbambali ambazo unakutana nazo kwenye uwanja wa tweet na baadae utaweza kuzisoma tweet hizo zikiwa kwenye mpangilio maalum ikiwa pamoja na njia mpya ya kushiriki na watu wengine.
Kingine kizuri kuhusu sehemu hii ni kuwa, pale utakapo hifadhi tweet hizo kwenye sehemu hiyo hakuna mtu mwingine ataweza kuziona, yaani hapa nina maana kuwa list ya tweet ulizo hifadhi inakuwa ni ya kwako pekee na hakuna mtu mwingine anaye weza kuona kitu ulicho hifadhi.
Vilevile Twitter inaleta kitufe kipya cha sehemu ya kushare ambacho kitakuwa badala ya kitufe cha sasa ambacho kipo kama bahasha, Twitter imeandika kwenye ukurasa wake kuwa maboresho haya yana tegemewa kuja kwenye programu za twitter za Android, iOS, Twitter Lite, pamoja na tovuti ya simu ya Twitter.