Baada ya mapambano ya muda mrefu sana sasa Twitter imeamua kufungua kimya kimya akaunti kwenye mtandao wa Instagram. Akaunti hiyo ambayo imeanzishwa siku ya ijumaa inatumiaka na Twitter kutangaza mtandao huo wa Twitter.
Kwa wale wasiojua kuhusu tofauti za Twitter na Instagram zilianza pale facebook ilipochukua baadhi ya sehemu ambazo zilitangazwa kwanza na twitter. Tofauti zao ziliendela mpaka kwenye instagram baada ya twitter kuzuia matumizi ya API zake kutumika kwenye mtandao huo wa instagram, Haikuishia hapo Instagram nayo pia ilisitisha matumizi ya API zake kwenye mtandao wa Twitter na kusababisha picha kuacha kutokea kwenye post zinazotoka kwenye instagram na ndipo mvutano huo ulipojulika rasmi kwa watumiaji wa mitandao hiyo.
Kwa sasa wataalamu wa mambo ya teknolojia wanasema kuwa inawezekana akaunti hiyo mpya itakuwa kwaajili ya kufanya matangazo tu na sio vinginevyo. Kwa upande mwingine wataalamu hao wanasema twitter haijafanya maamuzi sahihi kwani Twitter imeonekana kushindwa kiasi cha kuhitaji sana Instagram ili kupata watumiaji wapya.
Kwa Habari zaidi za teknolojia, endelea kutembelea Tanzania Tech au Download App ya Tanzania Tech ili kupata habari pindi zitakapo toka pia unaweza kujiunga na mtandao wetu wa Youtube ili kujifunza na kupata habari zote kwa njia ya video.