Mtandao wa Twitter hivi karibuni ulitangaza kuanza kufanya majaribio ya sehemu mpya ya Spaces, sehemu ambayo inaruhusu watumiaji kujiunga kwenye mazungumzo mbalimbali ya sauti ambayo huwa na muungano wa jumla ya watu 10.
Kupitia mazungumzo hayo, mtu yoyote anaweza kujiunga na kuwa msikilizaji au kuchangia mada inayozungumzwa moja kwa moja.
Sasa baada ya majaribio ya muda, hatimaye Twitter kupitia blog yake leo imetangaza kuleta sehemu hii kwa kila mtumiaji wa mtandao wa Twitter mwenye followers zaidi ya 600. Kupitia app ya Twitter akaunti yenye idadi hiyo ya followers itaweza kutengeneza Space na kualika watu moja kwa moja, au mtu yoyote yule ambaye ana follow akaunti hiyo anaweza kujiunga na kusikiliza.
Sehemu hiyo ya Space itakuwa inapatikana kwa juu sambamba na fleets ambapo Space zenyewe zitakuwa na duwara la rangi ya pink.
Kama unataka kujiunga na Space yoyote moja kwa moja bofya Space yenye mduara wa rangi ya pink, kisha moja kwa moja utaweza kujiunga na kusikiliza au kuchagua mada kama utapewa mwaliko wa kuwa mchangiaji au msikilizaji.
TABLE OF CONTENTS
Jinsi ya Kutengeneza Space
Kama unataka kutengeneza Space, moja kwa moja hakikisha akaunti yako inayo followers zaidi ya 600, kisha moja kwa moja update app ya Twitter kupitia play store au app store na baada ya hapo bofya sehemu ya kuandika Tweet na utaona sehemu mpya ya Space.
Andika jina la Spaces, kisha moja kwa moja bofya start your space, kwa kufanya hivyo moja kwa moja unatakiwa kuruhusu mic ya simu yako kupitia app ya Twitter na moja kwa moja utaweza kuanza kuzumza baada ya kuhakikisha sehemu ya mic ipo on.
Jinsi ya Kualika Watu Kuongea
Baada ya kutengeneza Space unaweza kualika watu kuchagia kwa kubofya sehemu ya mtu kisha chagua jina la mtu ambaye unataka aweze kuchagia kwenye Space yako.
Pia unaweza kuzuia baadhi ya watu kusikiliza na pia unaweza kukubali maombi ya watu kusikiliza moja kwa moja, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hapo chini.
Mbali ya hayo yapo mambo mengine mengi ambayo unaweza kufanya kupitia sehemu hii ya Space, na unaweza kutembelea tovuti ya Twitter kujua zaidi kuhusu sehemu hii mpya.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutangaza biashara kupitia mtandao wa Twitter.