Mtandao wa Twitter leo umetangaza rasmi kuwa sasa jina au username halita hesabiwa kwenye idadi ya maneno 140 ambayo unatakiwa kupost kwenye tweet moja kwenye mtandao huo.
Twitter imeamua hayo kama hatua ya kutekeleza kile ilicho ahidi cha kuboresha zaidi mtandao huo. Mwaka jana kampuni ya twitter ilitangaza kuondoa picha pamoja na link kwenye hesabu ya maneno 140 ambayo unatakiwa kupost kwenye tweet moja.
Hata hivyo wadau wengi wa teknolojia wanasema hii ni hatua nzuri ingawa bado mtandao huo una sheria nyingi hasa kwenye kupost tweet kwani inakuitaji kutengeneza maneno 140 tu ili kufikisha ujumbe unao utaka hii kuna wakati ni ngumu sana na inapelekea watu wengi kutumia mitandao mingine ya kijamii kufikisha taarifa kwa undani.
Twitter imethibitisha kuwa uwezo huo mpya wa kuondoa @usurname kwenye hesabu ya maneno 140 itanza kutumiaka hivi karibuni duniani kote kupitia programu za mtandao huo za Android pamoja na iOS. Kama unataka kujiaribu hii update programu yako ya Twitter kisha jaribu kumtag mtu kwenye tweet yako kisha angalia idadi ya maneno kwenye Tweet yako.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.