Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa “X”

Kwa mujibu wa Mask, Twitter inategemea kuanza kutumia nembo mpya ya “X”
Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa "X" Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa "X"

Kampuni ya Twitter huenda ikabadilishwa muonekano wake hivi karibuni na itakuwa inaitwa “X”, huku ikipatikana kupitia domain ya x.com.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya habari, mmiliki wa mtandao wa Twitter Elon Masks alitangaza hapo jana (Jumapili July 23, 2023) kuwa hivi karibuni mtandao huo utabadilishwa kabisa na nembo yake maarufu ya ndege wa rangi ya blue na sasa itabadilishwa na kuwa alama ya X.

Advertisement

Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa "X"

Kwa mujibu wa Mask, Twitter inategemea kuanza kutumia nembo hiyo mpya ya “X” kuanzia siku ya leo (tarehe 24 july 2023).

Musk, ambaye alinunua tovuti ya Twitter kwa dola bilioni 44 (Zaidi ya Trilioni 100 za Tanzania) mwezi wa Oktoba mwaka jana, aliandika kwenye Twitter mapema siku ya Jumapili kwamba ana nia ya kubadilisha nembo ya ndege wa bluu na kuwa nembo ya “X” kuanzia Jumatatu.

Musk alibadilisha jina rasmi la kampuni ya Twitter mwezi wa Aprili na kuwa X Holdings Corp, ili kufafanua wazo lake la kujenga “X, programu kamili” ambayo itatoa huduma za mitandao ya kijamii pamoja na malipo, kama ilivyo kwa WeChat ya nchini China.

Kwa mujibu wa watumiaji mbalimbali wa mtandao wa twitter, bila shaka mabadiliko hayo yakitokea yatawachanganya watumiaji wengi ambao tayari walikuwa ni watumiaji wa mtandao huo kwa muda mrefu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, Linda Yaccarino, alithibitisha uzinduzi wa nembo ya X siku ya Jumapili. Alituma ujumbe kwenye Twitter akisema: “Ni jambo la kipekee sana – katika maisha au biashara – kupata nafasi ya pili ya kuchangia mabadiliko makubwa. Twitter ilifanya mabadiliko makubwa na kubadilisha jinsi tunavyowasiliana. Sasa, X itaendelea mbele zaidi, na kufanya mabadiliko makubwa zaidi.”

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use