Tweet ya Obama Yawa Maarufu Zaidi Kwenye Historia ya Twitter

Tweet maarufu kuliko zote sasa kwenye mtandao wa Twitter
Obama Obama
Picha na Pete Souza/The White House

Mtandao wa Twitter ndio chombo cha mawasiliano kinacho pendwa sana na rais Trump, lakini ni chapisho la mtandao wa Twitter la rais wa zamani wa marekani Baraka Obama ndilo ambalo limependwa zaidi katika historia ya Twitter.

Tweet hiyo ambayo imemuonyesha raisi huyo wa zamani baraka obama akiwa anacheka na kundi la watoto wenye rangi tofauti huku akinukuu maneno kutoka kwa mwasisi na raisi wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela.

Advertisement

Hata hivyo Tweet yake hiyo tayari mpaka imependwa mara milioni 2.8, ikiwa imeipita tweet ya awali iliyokuwa inaongoza kwa kupendwa ya Ariana Grande alipotuma salamu za rambirambi baada ya shambulio la kigaidi la Manchester ‘Taught to Love’ (Nilifunzwa kupenda).

Picha hiyo inaonyesha ziara ya bwana Obama 2011 katika kituo cha kuangalia watoto katika eneo la Bethesda, mjini Maryland, Picha hiyo ilipigwa na aliyekuwa mpigia picha wa Ikulu Pete Souza ambaye Tangu ushindi wa rais Trump, amekuwa akichapisha picha katika Instagram zinozo onyesha uongozi wa bwana Obama akiufananisha na mrithi wake.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : The Guardian

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use