Baada ya jana kuangalia list ya video zilizo angaliawa zaidi kwenye mtandao wa YouTube, leo ni zamu ya Twitter na leo ninakuletea akaunti mbalimbali za twitter zilizofanya vizuri ikiwa pamoja na tweet mbalimbali ambazo zimefanya vizuri.
Kupitia makala hii tuta angalia vipengele mbalimbali ikiwa pamoja na tweet zilizopata retweet nyingi duniani, watu walio zungumziwa sana kupitia twitter mwaka 2020, pamoja na vipengele vingine vingi. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Retweet Nyingi Zaidi Mwaka (2020)
Kwa mujibu wa Twitter, tweet iliyopata retweet nyingi kuliko zote kwenye mtandao wa twitter ni tweet kutoka kwenye akaunti ya aliyekuwa muigizaji na muandaaji wa filamu maarufu Chadwick Boseman, ambaye alifariki mwezi wa 8 kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani. Tweet hiyo ndio iliyokuwa inatangaza kifo chake hapo tarehe 29 mwezi wa nane mwaka 2020. Chadwick Boseman alijulikana zaidi kutokana na movie yake ya Black Panther ya mwaka 2018. Hadi sasa tweet hiyo inayo retweet zaidi ya Milioni 2.4
Tweet yenye Likes Nyingi (2020)
Tweet yenye retweet nyingi kuliko zote kwenye mtandao wa twitter kwa mwaka 2020, ndio tweet yenye likes nyingi kuliko zote kwenye mtandao wa Twitter. Hadi sasa tweet hiyo inayo likes zaidi ya milioni 7.6. Tweet hiyo ndio tangazo la kifo cha msanii wa filamu Chadwick Boseman aliye igiza filamu ya Black Panther ya 2018.
Timu za Michezo Zilizo Ongelewa Zaidi Twitter (2020)
Kwa mujibu wa Twitter, timu ya mpira wa kikapu ya Lakers ndio imeonekana kuongelewa zaidi kwenye mtandao wa Twitter kwa mwaka 2020, ikifuatiwa na timu ya mpira wa miguu ya Manchester United.
Watu Walio Ongelewa Zaidi Twitter (2020)
Kwa mujibu wa Twitter, akaunti au watu walio ongelewa zaidi kwenye mtandao wa Twitter kwa mwaka 2020 ni pamoja na aliyekuwa raisi wa Marekani Donald Trump, huku ikifuatiwa na akaunti ya raisi wa sasa wa Marekani Joe Biden.
Emoji Zilizotumiwa Zaidi Twitter (2020)
Kama unavyoweza kuona hapo juu, emoji iliyo ongoza kwa kutumiwa zaidi mwaka 2020 kwenye mtandao wa Twitter ni pamoja na Emoji ambayo inajulikana kama “Face with Tears of Joy Emoji” ikifuatiwa na Emoji ya “Loudly Crying Face Emoji”.
Kwa mujibu wa Twitter na hayo ndio baadhi ya matukio ikiwa pamoja na Tweet na akaunti zilizofanya vizuri kwa mwaka 2020. Kama unataka kujua zaidi kuhusu 10 bora za mwaka 2020 hakikisha una endelea kutembelea Tanzania tech.
Kwa sasa bado hakuna list ya Tanzania, tunaendelea kufuatilia list yoyote ya Tanzania kwenye mtandao wa Twitter na tutakuletea habari zadi hivi karibini, endelea kutembelea Tanzania tech.