Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1

Fahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya TV mpya za Infinix S1
Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1 Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1

Kama tetesi zilivyosema siku za karibuni, hatimaye hapo jana kampuni ya Infinix ilizindua TV yake ya kwanza ya Infinix TV S1 huko nchini Nigeria. TV hii mpya ya Infinix TV S1 ni utambulisho wa brand ya Infinix kuingia rasmi kwenye biashara ya TV, huku brand ya TECNO pia ikitarajiwa kuja na TV yake baadae mwaka huu.

TV hii mpya ya Infinix inakuja kwa matoleo mawili tofauti, toleo la Infinix TV S1 ya Inch 43 na Infinix TV S1 ya inch 55. TV zote ni Smart TV na zinaendeshwa na mfumo wa Android huku zikiwa na uwezo wa kuunganishwa kwenye Internet, pamoja na uwezo wa kupakua programu mbalimbali za Android.

Advertisement

Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1

TV hizi zinakuja na resolution ya pixel 1920 kwa 1080 kwa TV ya Inch 43, na pixel 3840 kwa 2160 (4K) kwa TV yenye inch 55. TV zote zinakuja na uhifadhi wa ndani wa GB 8 pamoja na RAM ya GB 1 kwa TV ya inch 43 na GB 1.5 kwa TV yenye inch 55. Mbali na hayo TV hizi zinakuja na kioo chenye brightness ya hadi 250nits typ kwa TV ya inch 43 na 300 nits typ kwa TV ya inch 55.

Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1

Kwa upande wa muundo TV hizi zimetengenezwa kwa muundo wa Metallic design, huku kioo cha TV hizo kikiwa kimejaa kutokana na kingi nyembamba za TV hiyo (full screen). Kwa upande wa viunganishi TV hii inakuja na sehemu za HDMI mbili kwa TV ya inch 43 na HDMI tatu kwa inch 55.

TV hizi zote zinakuja na Bluetooth 4.0, Wi-Fi pamoja na Wi-Fi Direct bila kusahau HOTSPOT screen mirroring ambayo inakusaidia kuunganisha simu yako ya Infinix kwenye TV hiyo moja kwa moja. Pia unaweza kutumia simu yako ya Infinix kama E-remote au Air-mouse kwa kutumia app ya Infinix life app.

Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1 Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1 Hatimaye Infinix Yazindua TV Yake ya Kwanza Infinix TV S1

Sifa za Infinix Smart TV S1

Infinix TV S1 (43 inch) S1 (55 inch)
Resolution 1920 x 10803840 x 2160
RAM / ROMRAM GB 1 / ROM 8GBRAM GB 1.5 ROM 8GB
Brightness250 nits typ 300 nits typ
MuundoMetallic design, full screenMetallic design, full screen
Mfumo Endeshi Android Android
CastHotspot mirroringHotspot mirroring
Uwezo wa Speaker 2*10W2*10W
Product Warranty 24M 24M

Bei ya Infinix Smart TV S1

Kwa upande wa bei TV hizi mpya zinakuja zikiwa zinauzwa kwa bei nafuu huku zote zikiwa zinapatikana kwa ununuzi hapa Afrika. Infinix TV S1 ya inch 43 inauzwa kwa Naira N93,900 ambayo ni sawa na TZS 561,000. Kwa upande wa Smart TV ya inch 55 yenyewe itapatikana kwa Naira N152,000 sawa na TZS 910,000.

Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika pale TV hizi zitakapo zinduliwa hapa nchini Tanzania. Kuhusu upatikanaji TV hizi kwa sasa zinapatikana nchini Nigeria huku zikitarajiwa kuja nchini Tanzania wiki zijazo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use