Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Kama wewe ni mpenzi wa TV za Aboder basi hizi hapa TV za Aborder za bei nafuu
Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000 Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Katika hali ya kawaida ni wazi kuwa kila mtu anahitaji kutunza fedha na kununua bidhaa za bei nafuu, kuliona hili leo nimekuletea list ya TV za Aborder za bei rahisi ambazo unaweza kununua hivi sasa kwa bei ya chini ya TZS 300,000.

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Advertisement

Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kulingana na eneo ulilopo hivyo hakikisha unajiandaa vizuri kabla ya kwenda kununua TV hizo. Pia ni muhimu kufahamu TV unayo hitaji kwani hii itakusaidia kuweza kuweza kufanya uchaguzi sahihi.

Aborder Solar TV inch 17 (ABT 1722) – TZS 165,000

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Aborder Solar TV inch 17 (ABT 1722) hii ni TV nzuri ambayo inatumia mfumo wa umeme wa jua au Solar, TV hii ni bora sana hasa kwa sehemu ambazo hazina umeme wa uhakika. Mbali na hayo TV hii inakuja na sifa mbalimbali kama vile kioo kikubwa cha Inch 17, sehemu ya kuchomeka USB, sehemu ya HDMI, pamoja na teknolojia ya kutunza umeme au Energy Saving. Unaweza kupata TV hii ya Aborder kwa bei kati ya TZS 265,000 hadi TZS 165,000.

Aborder Solar TV Inch 15 (ABT 1522) – TZS 145,000

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Aborder Solar TV Inch 15” (ABT 1522) ni TV nyingine ya bei rahisi kutoka kampuni ya Aborder, TV hii ni kama TV hapo juu na inakuja na uwezo wa kutumia mfumo wa Solar, kioo cha inch 15 pamoja na sehemu ya kuchomeka USB, sehemu ya HDMI, pamoja na teknolojia ya kutunza umeme au Energy Saving. TV hii inapatikana hapa nchini Tanzania kwa bei kati ya TZS 190,000  hadi TZS 145,000.

Aborder Solar TV inch 22 (ABT 22D) – TZS 195,000

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Aborder Solar TV inch 22 (ABT 22D) ni TV nyingine ya Aborder ya bei rahisi, TV hii inakuja na muonekano mzuri na sifa kama ifuatavyo. TV hii inakuja na kioo cha inch 22, sehemu ya kuchomeka USB, sehemu ya HDMI, pamoja na uwezo wa kutunza umeme yaani Energy Saving. TV hii pia inao uwezo wa kutumika kupitia umeme wa jua maarufu kama Solar. Unaweza kupata TV hii kwa bei rahisi kati ya TZS 295,000 hadi TZS 195,000.

Aborder Solar TV Inch 19 (ABT 1922) – TZS 175,000

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Kama ilivyo TV nyingine hapo juu, Aborder Solar TV Inch 19 (ABT 1922) ni TV nyingine ya Inch 19 ambayo inapatikana kwa bei rahisi sana. TV hii inakuja na sifa zinazo fanana na TV hapo juu lakini yenyewe inakuja na kioo kidogo zaidi cha Inch 19. TV hii inafaa zaidi kwenye vijiji ikiwa pamoja na sehemu ambazo hazina umeme wa uhakika. Unaweza kuipata TV hii kwa bei kati ya TZS 275,000 hadi TZS 175,000.

Aborder Solar TV inch 24 (ABT 2448) – TZS 270,000

Hizi Hapa TV za Aborder za Bei Rahisi Chini ya TZS 300,000

Aborder Solar TV inch 24 (ABT 2448) ni TV nyingine ya Aborder ya bei nafuu ambayo unaweza kuipata kwa hapa Tanzania. TV hii inakuja na muonekano mzuri na inakuja na sifa kama ifuatavyo. Aborder Solar TV inch 24 (ABT 2448) inakuja na kioo cha inch 24, sehemu ya HDMI, USB pamoja na teknolojia mpya ya kutunza umeme ambayo inafanya TV hii kuweza kutumika kwa kutumia umeme unao zalishwa na solar au maarufu kama Solar. Unaweza kupata TV hii kwa kati ya TZS 360,000 hadi TZS 270,000.

Na hizo ndio TV za Aborder za bei rahisi, kumbuka bei ya TV hizi inaweza kubadilika kulingana na eneo ulilipo hivyo ni vizuri kujipanga vizuri pale unapokwenda kununua.

Kama unataka kujua zaidi ni TV gani ununue kwa kuangalia ukubwa wa chumba chako unaweza kusoma hapa mambo unayotakiwa kufahamu kabla ya kununua TV. Kama unataka bidhaa nyingine zaidi za bei rahisi hakikisha unendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use