Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65)

Hii hapa TV Mpya ya OLED ya kisasa kutoka kampuni ya Huawei
Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65) Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65)

Kama ilivyo kampuni ya Nokia, kampuni ya Huawei hivi karibuni imeingia kwenye biashara ya TV na hivi karibuni kampuni hiyo imezindua TV yake ya kwanza ya OLED.yenye Inch 65.

Advertisement

Kwa mujibu wa Huawei, TV hiyo mpya inakuja na kioo cha kisasa cha OLED chenye uwezo wa refresh rate hadi 120Hz huku ikiwa inasaidiwa na teknolojia nyingine kama HDR pamoja na uwezo wa hadi nits 1,000 za brightness.

Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65)

Mbali na ubora wa kioo cha TV hiyo, TV hiyo pia inasemekana kuja na spika za kisasa zaidi ya 13 spika ambazo zipo nyuma ya TV hiyo. Hata hivyo spika hizo kwa ujumla zinasemekana zinaweza kuzalisha sauti yenye nguvu hadi Walt 75.

Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65)

Hata hivyo mbali na TV hiyo kuwa na spika nyingi pengine kuliko TV ambazo umezoea, TV hii pia inakuja na kamera ambayo imejificha kwa juu, kamera ambayo inasemekana kuja na uwezo wa Megapixel 24 ambayo pia ni ultrawide-angle lens. Kamera hiyo inaendeshwa na mota maalum ambapo inaweza kujificha kabisa kwenye sehemu ya juu ya TV hiyo.

Huawei Yazindua TV Yake ya Kwanza ya OLED (Vision X65)

Kamera hiyo inasemekana kuendeshwa na chip ya Huawei ya HiSilicon Hi3559C chipset ambayo inakuja na uwezo wa AI au Artificial Intelligence. Pia kamera hiyo inasemekana kuwa na uwezo wa kusaidia mtumiaji kuendesha vitu mbalimbali kwenye TV hiyo bila kugusa TV hiyo au bila kutumia remote kama ilivyo zoeleka. Mtumiaji ataweza kutumia ishara mbalimbali kuweza kuendesha baadhi ya sehemu kwenye TV hiyo, kama vile kusogeza mbele nyimbo au video pamoja na kuongeza sauti au kupunguza.

Kwa upande wa sifa za ndani, TV hii mpya ya OLED kutoka Huawei inakuja na processor ya Honghu 898 chip ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 128. Processor hiyo pia inakuja na teknolojia ya AI hivyo tegemea kuwa TV hii itakuwa na mambo mengi sana ambayo TV ya kawaida haito weza kufanya.

Kwa upande wa bei, TV hii mpya ya Huawei itaingia sokoni kuanzia tarehe 26 mwezi huu huku ikiwa inauzwa kuanzia dollar za marekani $3,500 ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania TZS 8,100,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use