Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Bei ya TV hizi haizidi Shilingi za kitanzania 400,000
Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000 Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye mpango wa kununua TV mwaka huu 2019 basi habari njema kwako kwani leo nimekukusanyia list ya TV bora za bei nafuu ambazo unaweza kununua sasa kwa chini ya Tsh 400,000. Kumbuka TV zote kwenye list hii zinapatikana hapa Tanzania na baadhi ya nchi za jirani kama vile Kenya na Uganda.

Baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tukangalie TV hizi, kumbuka pia unaweza kununua TV hizi mtandaoni kwa kubofya link husika chini ya maelezo ya TV, basi bila kupoteza muda wako zaidi twende tukangalie TV hizi.

Advertisement

Samsung T24E310MX

Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Sifa za TV 

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 23.6
  • Uwezo wa Kuonyesha Channel Bila Kingamuzi – Ndio
  • Aina ya TV – VA LED TV
  • Resolution – 1366 x 768
  • Sehemu ya HDMI – Zipo mbili
  • Sehemu ya USB – Ipo Moja

Kama wewe mpenzi wa TV za Samsung na ulikuwa unataka TV ya bei nafuu yenye uwezo wa kuonyesha channel za ndani bure bila kingamuzi au kisimbusi basi TV hii kutoka kampuni ya Samsung ni bora sana kwako, TV hii mbali ya kuja na uwezo wa kuonyesha TV pia inakuja na sehemu mbili za HDMI ambazo zinaweza kukupa uwezo wa kutumia kompyuta au hata kifaa kingine chenye uwezo wa HDMI.

NUNUA HAPA KWA TSH 354,000

LG 24MT48DFHizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Sifa za TV 

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 23.6
  • Uwezo wa Kuonyesha Channel Bila Kingamuzi – Ndio
  • Aina ya TV – LED TV
  • Resolution – 1366 x 768
  • Sehemu ya HDMI – Zipo mbili
  • Sehemu ya USB – Ipo Moja

Kama wewe ni mpenzi wa TV ambayo ina uwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja basi TV hii ni nzuri sana kwako, TV hii inakuja na uwezo wa kuunganisha Game, pia inakuja na Game zake ndani yake. TV hii ya LG ni nzuri sana kwa mtu ambaye haitaji kuwa na kisimbusi kwani inakuja na uwezo wa kuonyesha channel za ndani bure bila kulipia. TV hii pia inayo HDMI pamoja na sehemu ya USB ambayo unaweza kutumia kuangalia Movie moja kwa moja kutoka kwenye Flash au External Hard Disk.

NUNUA HAPA KWA TSH 345,000

Toshiba S1710EE

Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Sifa za TV 

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 32
  • Uwezo wa Kuonyesha Channel Bila Kingamuzi – Hapana
  • Aina ya TV – HD D-LED TV
  • Resolution – 1366 x 768
  • Sehemu ya HDMI – Zipo mbili
  • Sehemu ya USB – Zipo Mbili

Kama wewe ni mtu ambaye unapenda kuangalia filamu au kusikiliza muziki basi TV hii itakufaa sana. TV hii ni nzuri sana kwani inakuja na sehemu mbili za kuchomeka Flash, sehemu ambazo zina uwezo wa kusoma filamu na muziki. Pia inayo sehemu za HDMI mbili ambazo unaweza kutumia kuunganisha kompyuta yako au kisimbusi chenye sehemu hizo kama DSTV na Azam TV, Tofauti iliyopo kwenye TV hii ni kuwa haina uwezo wa kuonyesha TV za ndani bila kuwa na kingamuzi hivyo ni lazima kuwa na kingamuzi kama utanunua TV hii.

NUNUA HAPA KWA TSH 365,000

Rising RS 32A30 LED

Hizi Hapa TV Nzuri za Bei Nafuu Chini ya Tsh 400,000

Sifa za TV 

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 32
  • Uwezo wa Kuonyesha Channel Bila Kingamuzi – Bado Haija Julikana
  • Aina ya TV – LED TV
  • Resolution – 1920×1080
  • Sehemu ya HDMI – Ipo Moja
  • Sehemu ya USB – Ipo Moja

Kama wewe ni mmoja wa wapenzi wa vifaa vya Rising basi TV hii ni nzuri sana kwako, TV hii inakuja na kioo kikubwa chenye Resolution kubwa na pia TV hii inakuja na teknolojia za kisasa kwani hii ni Smart TV. Kwa wale ambao hamjui Smart TV hizi ni zile TV ambazo unaweza kuingia kwenye Internet na pia unaweza kudownload programu mbalimbali kupitia TV yako, mbali na hayo unaweza kuangalia Filamu na TV kupitia app za kudownload kama Netflix pamoja na iFlix ambayo ina ushirika na kampuni ya simu ya Vodacom.

NUNUA HAPA KWA TSH 400,000

Update Tarehe 2/4/2019 : Baada ya baadhi ya TV kununuliwa na nyingine kupandishwa bei ghafla tumeamua kuondoa link za kununua TV hizi kwani bei yake inaweza kupandishwa muda wowote.

Kwa sasa hizo ndio TV ambazo nimefanikiwa kuzipata ambazo zinauzwa hapa Tanzania sio zaidi ya Tsh 400,000. Kumbuka zipo TV nyingi sana zinazouzwa chini ya bei hii lakini kama kichwa cha habari kinavyosema hizi ni TV bora ambazo unaweza kuzipata kwa bei hiyo. Unaweza kununua TV kwa kubofya link nilizokuwekea chini ya maelezo ya TV.

Kama unataka kujua TV nyingine za bei kama hii hakikisha unatembelea ukurasa huu kila mara kwani tutakuwa tunaongeza TV nyingine pindi tutakapo ona TV ina ubora unastahili. Kwa habari zaidi za teknolojia usiache kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

6 comments
  1. Sina Maoni ila ninataka kujua maduka yetu ya tv kwa upande wa morogoro, au uparikanaji wa bidhaa yetu kwa upande wa morogoro

  2. Swali langu ni je kwa hizi tv znazoonyesha channel bila kingamuzi kuna sehem ya CI card, je ikiwekwa hyo card na ikalipiwa inaweza kuonyesha channel zotee? Na je hyo CI card huwa inanunuliwa pembeni au inatoka pamoja na tv

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use