Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Yazindua TV ya Kwanza yenye Uwezo wa 8K

Hii ndio TV ya kwanza ya Samsung yenye 8K itakayo wafikia wateja duniani kote
TV ya Kwanza Samsung yenye 8K TV ya Kwanza Samsung yenye 8K

Hivi karibuni kampuni ya Samsung kuptia mkutano wa IFA 2018 imetangaza ujio wa TV yake ya kwanza yenye teknolojia ya 8K. TV hii sio ya kwanza kutengenezwa na Samsung yenye teknolojia ya 8K lakini ni TV ya kwanza kabisa ambayo itakuwa inauzwa kama TV za kawaida, yaani kifupi ni kuwa hii ndio TV ya kwanza ya 8K kutoka Samsung itakayo wafikia wateja mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa Samsung TV hiyo yenye model namba Q900R, itawafikia wateja wa baadhi ya nchi kuanzia mwezi ujao na inasemekana kuwa TV hiyo itakuja na teknolojia ya AI moja kwa moja kutoka kwenye box. Mbali na hayo TV hiyo inasemekana kuwa na uwezo wa kuonyesha picha angavu hadi kufikia brightness ya 4,000 nits, huku ikiwa inakuja na teknolojia mpya ya HDR10+ ambayo hii ni zaidi ya HDR au (High Dynamic Range).

Advertisement

Sasa kama ulikuwa unajiuliza mfumo wa AI unafanya nini kwenye TV hii, Kwa mujibu wa Samsung mfumo huo wa AI ambao kwa kitaalamu unaitwa “8K AI Upscaling” utakuwa unafanya kazi ya kubadilisha picha ambazo sio zenye mfumo wa 8K na kuzifanya ziwe na muonekano angavu ambao utakuwa unalingana na mfumo wa 8K bila kujali format ya picha au video zilivyo chukuliwa hapo awali. Kufikia matokeo hayo, TV hiyo mpya ya Samsung Q900R 8K hutumia mfumo huo pamoja na processor ya TV hiyo ya (Quantum Processor 8K).

Kwa sasa bado hakuna taarifa za ujio wa TV hii kwenye nchi zingine, pia bado kampuni ya Samsung haijatangaza rasmi bei ya TV hii. Kama unataka kujua zaidi kuhusu TV hii mpya ya 8K kutoka Samsung endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use