Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

TV 10 Bora za Kununua Zenye Teknolojia ya 4K Mwaka 2017

Hizi hapa ndio TV bora zenye 4K mwaka huu 2017
TV Bora za 4k Mwaka 2017 TV Bora za 4k Mwaka 2017

Ni muda mrefu umepita toka tuongelee kuhusu maswala ya TV, lakini kizuri ni kwamba kutokana na  ukimya huo sasa yapo mambo mengi sana ya kukufahamisha kuhusu TV. Na kwa kuanza siku ya leo ningependa tuangalie TV bora zenye teknolojia ya 4K ambazo unaweza kununua kwa mwaka huu 2017.

Tuki zungumzia kidogo kuhusu teknolojia ya 4k. 4K ni neno la kiteknolojia linalotumika kuelezea kuhusu kioo cha tv chenye mkusanyiko wa jumla wa pixel ambao ni mara 4 zaidi ya pixel zinazopatikana kwenye kioo cha tv yenye Full HD, Kujua zaidi kuhusu 4K BOFYA HAPA.

Advertisement

Baada ya kujua hayo machache kuhusu teknolojia ya 4K basi moja kwa moja twende tukangalie TV hizi bora kabisa za kununua mwaka huu 2017 zenye teknolojia ya kisasa ya 4K au UHD.

10. Panasonic DX750

TV hii inakuja kwa ukubwa wa aina tatu inakuja ikiwa na ukubwa wa inch 50, 58 pamoja na 65. TV hii pia inakuja na teknolojia ya Smart TV huku ikiwa na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwenye mtandao.

9. Sony XE93 series

TV hii inakujua kwa ukubwa wa aina mbili tofauti TV hii inakuja kwa ukubwa wa inch 55 pamoja na Inch 65. Kwa upande wa teknolojia TV hii sio SmartTV bali TV hii inauwezo mkubwa wa kuonyesha picha angavu huku ikitoa sauti ya kipekee pengine kuliko TV zote kwenye list hii, TV hii ni nyembaba sasa na ni bora kwa wanaopenda TV za aina hii.

8. Philips 65PUS7601

Hii ni moja kati ya TV bora sana zenye mfumo wa Smart TV, TV hii inakuja kwa ukubwa wa aina moja tu ambayo ni inch 65, TV hii inayo teknolojia ya Smart TV ambayo ina kuruhusu kuperuzi kwenye programu mbalimbali kwa kutumia mtandao.

7. LG OLED B7 Series

TV hii ni moja kati ya Tv zenye ubora mkubwa sana wa picha, TV hii inapatika kwa ukubwa wa aina mbili yani inch 55 pamoja na inch 65. TV hii inayo teknolojia ya HDR yenye kufanya ubora wa picha kwenye TV hii kubwa bora zaidi na zaidi.

6. Panasonic DX902 series

Hii ni moja kati ya TV bora na ya kisasa sana TV hii inapatikana kwa ukubwa wa inch 58 pamoja na 65, kwa upande wa teknolojia TV hii inayo teknolojia ya HDR impact yenye kufanya uweze kupata picha angavu sana.

5. Samsung KS7000 range

Ukiwaza kuwa na TV Bora na yenye uwezo mkubwa wa 4K basi hii ndio TV ya kununua, Tv hii ina kuja na ukubwa wa inch 49, 55, 60 pamoja na Inch 65. TV hii kwa upande wa teknolojia inakuja na teknolojia za kisasa pamoja na muonekano mzuri na wenye kutokuwa na pembe kubwa kiasi kuwa inafanya TV hii kuwa nyembamba sana.

4. Sony BRAVIA A1E OLED

Kama unatafuta TV yenye ubora wa hali ya juu pamoja na Souti basi TV hii ni moja kati ya TV bora sana kuwa nayo, TV hii inakuja kwa ukubwa wa inch 65 pamoja na inch 77. Kwa upande wa teknolojia TV hii inayo teknolojia ya Smart TV yenye kuweza kutumia programu mbalimbali kwenye mtandao.

3. Sony Bravia XE93 series

Kwa wapenzi wa TV bora na za kisasa basi hii ndio moja ya TV ambazo ni bora kabisa kuwa nayo TV hii inakuja kwa ukubwa wa inch 49, 55, 65 pamoja na inch 75. Kwa upande wa teknolojia Tv hii inayo teknolojia ya Smart TV huku ikiwa na ubora wa kisasa wa picha pamoja na muundo wake.

2. LG OLEDE7 series

Kwenye namba mbili ni LG OLEDE7 series ambayo hii ni TV ya kisasa na ina uwezo wa hali ya juu sana na ni moja kati ya TV nyembamba sana kwenye list hii TV hii inakuja na ubora wa hali ya juu huku ikiwa na teknolojia ya Smart TV.

1. Samsung Q9F QLED

TV hii ni moja kati ya TV bora sana na ukweli kuwa ni Bei ghali sana lakini kutokana na ubora wake bei yake inaendana kabisa na ubora wa TV hii. TV hii inayo teknolojia ya Smart TV pamoja na teknolojia nyingine nyingi na bora sana. TV hii inapatikana kwa ukubwa wa inch 65.

Na hizo ndio baadhi tu ya TV ambazo zinatumia teknolojia ya 4K na ambazo ni bora kununua kwa mwaka huu 2017. Kama unataka kujua TV bora za kununua kwa mwaka ulipita yaani 2017 basi SOMA HAPA.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

 Chanzo : Tech Radar

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use