Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu ya WhatsApp basi ni wazi kuwa umesha sikia kuwa whatsapp inakuja na sehemu mpya ambayo itaruhusu kutumia programu ya WhatsApp bila namba ya simu moja kwa moja.
TABLE OF CONTENTS
Linked Device ni nini
Sehemu hii inaitwa Linked Device, Linked Device ni sehemu mpya ambayo inaruhusu mtumiaji kuweza kuunganisha programu ya WhatsApp ambayo mtumiaji anatumia kwenye simu yake na kompyuta au kifaa kingine bila programu ya WhatsApp kuwa online kwenye simu.
Hapo awali ilikutumia programu ya WhatsApp kwenye kompyuta au kifaa kingine tofauti na simu na tablet, ilikuwa ni lazima kuhakikisha programu ya WhatsApp imewashwa kwenye simu yako na unatumia Internet kwenye simu yako ili kuendelea kutumia programu hiyo kwenye kompyuta.
WhatsApp Bila Namba (Linked Devices)
Ili kutumia sehemu hii unatakiwa kuhakikisha una update programu yako ya WhatsApp, (kwa sasa sehemu hii ipo kwenye majaribio hivyo unaweza usione sehemu hiyo baada ya ku-update). Baada ya hapo moja kwa moja bofya vidoti vitatu juu upande wa kulia, kisha chagua Linked devices.
Baada ya hapo utaona sehemu mpya ambapo utaona kitufe cha Link a device, bofya hapo kuendelea kuunganisha programu yako ya WhatsApp ili kutumia bila namba ya simu.
Baada ya hapo scan QR code mara ya kwanza, kisha rudia mara ya pili kwa kutumia simu yako kisha moja kwa moja utaona programu yako ya WhatsApp imeunganishwa na kompyuta yako au kifaa chochote unachotumia.
Baada ya hapo sasa utaweza kutumia programu ya WhatsApp bila simu yako kuwa imeunganisha na internet pale unapotumia WhatsApp kwenye kompyuta yako.
Mengine Kuhusu WhatsApp Linked Devices
Mambo mengine ambayo ningependa ufahamu kuhusu sehemu hii ni kuwa, usalama wa mtu kuunganisha WhatsApp yako na kuendelea kutumia bila wewe kujua ni mkubwa hivyo pengine kwa kuwa sehemu hii bado ipo kwenye majaribio WhatsApp inaweza kuboresha sehemu hii na kuonyesha pale mtu atakapo unganisha WhatsApp yako bila wewe kujua.
Vinginevyo binafsi naona sehemu hii ni nzuri kwangu hasa kwa sababu ya mimi muda mwingi natumia kompyuta hivyo pengine hii itasaidia kuendelea kuwasiliana na watu kwa urahisi hata kama simu yangu ipo mbali na mimi.
Nini maoni yako kuhusu sehemu hii..? Je unahisi sehemu hii ni bora kwako au unahisi itafanya usalama wako kuwa mdogo zaidi ukizingatia pia unaweza meseji zinakuja kwenye simu kama vile hazijasomwa.? Toa maoni yako kupitia sehemu ya maoni hapo chini.