Kama wewe ni mpenzi wa muziki ni wazi kuwa tayari unayo app ya Spotify kwenye simu yako kwa ajili ya kusikiliza nyimbo za wasanii mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mbali ya kuwa Spotify ni sehemu bora sana ya kusikiliza muziki, lakini pia inapatikana kwa kulipia na kama unataka kutumia bure lazima utakutana na matangazo ambayo kwa namna moja ama nyingine kuna wakati yanaweza kuwa sumbufu tena hasa wakati ambao una sikiliza muziki.
Sasa kuliona hili, leo nimekuletea makala ambayo itaweza kusaidia kuweza kutumia App ya Spotify bila matangazo au bila kusikia matangazo ambayo huwa yanapita baada ya muda fulani. Matangazo haya ni yale matangazo ya sauti.
Kwa kuanza ni vyema nikwambie kuwa njia hii inafanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android na sio iPhone au iOS. Kama unatumia simu ya iOS basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa maujanja hivi karibuni.
Basi kama unayo simu yako ya Android, moja kwa moja endelea kwenye makala hii.
Kwa kuanza install, programu kupitia link hapo chini. Kumbuka hakikisha tayari unayo app ya Spotify kwenye simu yako kabla ya kudownload app hii, Kama hauna install Spotify kwanza.
Baada ya kuinstall app hii, sasa rudi kwenye app ya Spotify na endelea kwa kubofya sehemu ya menu ya settings inayopatikana kwa alama ya cog au kipuli cha mashine.
Baada ya kubofya sehemu ya Settings kisha endelea kwa kutafuta sehemu iliyo andikwa “Device Broadcast Status” na washa sehemu hiyo kwa kuhakikisha ina alama ya kijani.
Baada ya hapo funga app ya Spotify kisha endelea kwa kufungua app uliyo download hapo awali na utakutana na switch bofya ili kuwasha switch hiyo.
Kama tayari ulisha fuata hatua za mwanzo utakuwa tayari kutumia Spotify bila matangazo ya sauti, kama utakuwa ujafuata hatua nilizo elekeza hapo juu, basi utaweza kuona pop up yenye kutaka uwashe sehemu ya “Device Broadcast Status” ambayo inapatikana kwenye Settings ya app ya Spotify, washa sehemu hiyo kwa kufuata maelezo hapo juu.
Njia Nyingine ya Pili
Ikiwa mbinu hapo juu haifanyi kazi kama ulivyo tarajia basi unaweza kuchagua toleo lililobadilishwa la Spotify ambalo hukupa baadhi ya vipengele vya kulipia bila malipo kama vile kusikiliza nyimbo bila kikomo, usikilizaji wa muziki bila matangazo, na uwezo wa chagua muziki wowote kutoka kwenye playlist yoyote.
Unaweza kudownload app hii ambayo imeondolewa matangazo na kubadilishwa kupitia link hapo chini. Hakikisha unachagua sehemu ya “DOWNLOAD APK FILE V8.6.32.925 MOD”.
Kwa kufuata njia zote hizi ni wazi kuwa lazima utaweza kutumia app ya Spotify kusikiliza muziki bure kabisa bila matangazo. Kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kuskip matangazo kwenye app ya YouTube bila kubofya sehemu yoyote wakati video inacheza.
Haya ni majaribio