Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tumia Simu Yoyote Android Kwa Haraka (Mkono Mmoja)

Tumia simu yenye kioo kikubwa kwa mkono mmoja mahali popote
Tumia Simu Yoyote Android Kwa Haraka (Mkono Mmoja) Tumia Simu Yoyote Android Kwa Haraka (Mkono Mmoja)

Kadri siku zinavyokwenda ndio simu zinazidi kuwa kubwa hasa kwenye upande wa kioo, hii inafanya inakuwa ni ngumu sana kutumia simu kwa mkono mmoja, kuliona hili leo Tanzania Tech tumekuletea njia rahisi ya kutumia simu yoyote ya Android kwa urahisi kwa mkono mmoja.

Njia hii ni rahisi sana na inaweza kumsaidia mtu yoyote kuweza kutumia simu ya Android kwa mkono mmoja bila kujali una maumbile ya mikono midogo au hata unayo mikono mikubwa. Basi kwa kusema hayo twende moja kwenye njia hii.

Advertisement

Kwa kuanza hakikisha simu yako inayo bando la kutosha kisha moja kwa moja ingia kwenye soko la Play Store na pakua app ya Quick Cursor, unaweza kupata app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya hapo sasa endelea kwa kufuatisha maelekezo kwenye video hapo chini, maelezo hayo ni rahisi lakini kwa maandishi ni ngumu kuelewa ndio maana ni lazima uangalie video hapo chini.

Kwa kufuata hatua zote hizo natumaini utakuwa umeweza kutumia simu yako ya Android kwa mkono mmoja kwa urahisi, Kama una mahali ambapo sijaeleweka unaweza unaweza kuniandikia kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Pia naomba radhi kwa sauti yangu leo ina mafua kidogo.

Kwa maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuangalia movie kutoka mtandao wa Netflix bure kabisa na bila kuwa na akaunti yoyote. Kwa maujanja zaidi kwa vitendo hakikisha una subscribe kwenye channel yetu hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use