Teknolojia imendela kubadilisha maisha yawatu kila siku lakini kama haitoshi teknolojia haijaishia hapo siku hizi simu yako ya mkononi inauwezo wa kufanya mambo zaidi ya yale ya kwaida ambayo tumezoea simu ya mkononi kufanya.
Hivi karibuni huko nchini marekani wataalamu kutoka kampuni ya Laan Labs wamefanikisha kutengeneza app ambayo itakusaidia kufanya vipimo vya urefu na upana kwa kutumia simu yako, wataalamu hao wamefanikisha hilo kwa kutumia mfumo na teknolojia mpya ya apple ya ARKit framework.
Katika video hiyo hapo juu kampuni hiyo imeonyesha jinsi app hiyo iliyo pewa jina la AR Measure jinsi inavyofanya kazi. Mtu ataweza kutumia kamera ya simu yake kuweza kuchukua vipimo vya urefu na kutokuwa na haja ya futi kwani vipimo huonekana juu ya kioo chako moja kwa moja.
Kwa sasa App ya AR Measure bado iko kwenye hatua za mwisho na siku za karibuni itaingia rasmi kwenye soko la mfumo wa iOS yaani App Store, kwa sasa unaweza kujisajili kwa kutumia barua pepe yako hapa ili kupata taarifa app hiyo itakapo patikana kwenye mfumo wa iOS. Kwa watu wanaotumia mfumo wa Android inabidi kusubiri kidogo ili kuweza kupata app hii ambayo pengine ni bora sana kwa watu mbalimbali.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.