Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja

App hizi zitakusaidia kutuma meseji kwa wateja wako au kikundi cha watu kwa haraka
Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja Apps za Kusaidia Kutuma SMS Nyingi kwa Pamoja

Kama wewe ni mfanyabiashara au labda unataka kutoa taarifa fupi kwa watu wengi kwa wakati mmoja ni wazi kuwa unahitaji SMS, japo kuwa kwa sasa kuna programu nyingi za kutuma ujumbe mfupi lakini ni wazi kuwa SMS bado inayo nafasi yake hasa kibiashara.

Kuliona hilo leo nimekuandalia apps ambazo zinaweza kusaidia kutuma meseji nyingi kwa pamoja kwa watu mbalimbali. Kumbuka baadhi ya apps hizi zina mfumo wa kulipia lakini app nyingi kwenye list hii ni app za bure kabisa na unaweza kutumia bila kulipia gharama yoyote.

Advertisement

Kitu cha muhimu usitumie njia hii vibaya na hakikisha unatuma meseji kwenye namba ambayo umepewa ruhusa ya kutumia, kumbuka ni kinyume na sheria kutuma ujumbe mfupi wenye nia yoyote mbaya kwa mtu. Hatuta husika kwa namna yoyote kama ukitumia njia hii vibaya. Njia hizi ni kwaajili ya elimu tu na sio vinginevyo.

Multi SMS Sender

Multi SMS Sender ni app ya kwanza kwenye list hii, app hii ni ya kwanza kwa kuwa ina kuja na uwezo ambao natumaini watu wengi wanaweza kuipenda zaidi. App hii inakuruhusu kutuma zaidi ya SMS 6,000 kwa wakati mmoja.

Download App Hapa

Kupitia app hii unaweza kutuma SMS kwenye magroup mbalimbali ya namba za simu ambayo unaweza kutengeneza ndani ya app, pia unaweza kutuma SMS kwa watumiaji wako bila kuhifadhi namba zao kwenye simu yako. Pia unaweza kuweka alama maalum kwenye SMS zako ikiwa pamoja na kuonyesha ripoti za SMS mbalimbali kama zimefika au kama hazijafika.

Bulk Sms Plans

Bulk SMS Plans ni app nyingine ambayo itakusaidia sana kutuma SMS kwa watu wengi kwa pamoja. App hii tofauti na app iliyo tangulia, yenyewe inakuja na mfumo wa kulipia na unaweza kutuma SMS kwa haraka kwa kutumia Internet.

Download App Hapa

Uzuri wa app hii ni kuwa unaweza kuchagua Jina la SMS litakavyo kuwa linaonekana pale watumiaji wako watakapo pokea SMS zako. Mbali na hayo, unaweza kutuma SMS 5,000 kwa wakati mmoja huku meseji hizo zikifika wakati huo huo kwa sababu zinatumwa kwa kutumia Internet. Kizuri kuhusu app hii ni kuwa unaweza kutengeneza Theme ya SMS kwa ajili ya kutuma kila wakati.

Group Messaging

Group Messaging ni app nyingine ya mwisho kwenye list hii, japokuwa app hii ni ya mwisho haina maana kuwa app hii ni mbaya. App hii inakuja na mfumo ambao ni rahisi kutumia kwa mtu yoyote na unaweza kutuma SMS kwa vikundi mbalimbali.

Download App Hapa

App hii inakuja na sehemu ya kutengeneza magroup au vikundi mbalimbali, kisha baada ya hapo unaweza kuandika meseji moja na kutuma kwa kikundi cha watu ambao utakuwa umewachagua. Kwa upande mwingine app hii ni nyepesi na inakuja na muonekano ambao sio mzuri sana lakini ni rahisi kutumia kwa mtu yoyote yule.

Na hizo ndizo app ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, app ambazo zinaweza kusaidia kutuma ujumbe mfupi au SMS kwa watu wengi kwa pamoja. Kama unataka kujua app nyingine zaidi unaweza kusoma hapa kujua programu zinazoweza kukusaidia kutafuta mafile kwa haraka kwenye kompyuta yako ya Windows 10.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use