Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti 6 Zinazoweza Kukusaidia Kupata Pesa Mtandaoni

Inawezekana kabisa ulikuwa hujui kuhusu tovuti hizi
tovuti zinazokupa pesa mtandaoni tovuti zinazokupa pesa mtandaoni

Katika duniani hii ya teknolojia ni wazi kuwa njia za kutafuta kipato zimekuwa zikibadilika kila siku, Kutafuta pesa mtandaoni ni moja kati ya njia kuu ambazo zinatumiwa na vijana wengi kote duniani ili kuweza kupata kipato cha kuendesha maisha ya kila siku.

Siku ya leo nimekuletea list ya tovuti ambazo zinaweza ku-kusaidia kuongeza kipato chako kwa kiasi kikubwa, kumbuka ni muhimu kujua kuwa hakuna kitu kirahisi duniani hivyo ni vyema kuweka malengo na kufanyia kazi tovuti hizi mara kwa mara ili uweze kuona mafanikio na kuweza kutengeneza kipato kinacho eleweka. Basi bila kupoteza muda twende tukaangalie tovuti hizi.

Advertisement

6. Uploadboy

uploadboy

Uploadboy ni tovuti inayoweza kukusaidia kupata pesa mtandao kwa namna ya kipekee, tovuti hii inakupa uwezo wa kuweza kupata pesa pale watu wengi zaidi watakapo download file ulilo upload kwenye tovuti hiyo. Unachotakiwa kufanya ni kujiunga kwa kubofya hapo chini, kisha upload file ambalo unataka watu waweze kudownload kisha share link hiyo na watu wako, kadri watu wanavyozidi kudownload ndivyo unavyozidi kupata pesa zaidi.

Bofya Hapa Kujiunga na Uploadboy

5. 000webhost

000webhost

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujipatia pesa kwa kuwa na tovuti ya bure kabisa basi tovuti ya 000webhost ni tovuti bora kwako. Tovuti ya 000webhost ni tovuti inayokupa uwezo wa kutumia web hosting bure kabisa bila kulipia, mbali na hayo unaweza kujipatia pesa mtandaoni kwa kualika watu kutumia huduma hiyo. Ili kujiunga unaweza kubofya hapa chini kujiunga na baada ya hapo bofya sehemu ya Earn Money kujiunga na huduma hiyo ya kupata pesa.

Bofya Hapa Kujiunga na 000webhost

4. Upload

upload

Upload ni tovuti nyingine ambayo itakulipa kutokana na idadi ya watu watakao download file lako, Tovuti hii inafanya kazi kama uploadboy na unaweza kupata kiwango kikubwa cha pesa kwa kutumia tovuti hii. Unaweza kujiunga na tovuti hii kwa kubofya hapo chini.

Bofya Hapa Kujiunga na Upload

3. TopBuzz

topbuzz

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda video za kufurahisha au kushangaza au hata pengine kuelimisha basi utaipenda TopBuzz. Topbuzz ni tovuti inayokupa nafasi ya kupata pesa kwa kuweka video zako fupi na kadri watu wanavyozidi kuangalia video zako basi ndivyo unavyozidi kupata pesa kwa haraka zaidi, unaweza kujiunga kwa kubofya hapo chini.

Bofya Hapa Kujiunga na TopBuzz

2. BeForward

beforward

Beforward ni moja kati ya kampuni kubwa sana ya uuzaji wa magari yaliyotumika hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Lakini pamoja na kuuza magari siku za karibuni be forward imeanzisha soko la vifaa vya kielektroniki kama vile simu za mkononi na vitu vingine kama hivyo. Kupitia vitu hivi vyote be forward inayo njia rahisi ya kuweza ku-kusaidia kupata pesa mtandaoni, unachotakiwa kufanya ni kujisajili na akaunti ya beforward supporters na utaweza kuwapa wateja wa beforward punguzo la bei na pia utaweza kupata pesa kwa urahisi sana.

Bofya Hapa Kujiunga na Beforward

1. PropellerAds

propellerads

Propeller Ads ni tovuti ambayo haina tofauti sana na Google Adsense, lakini uzuri wa tovuti hii ni kuwa unaweza kujipatia pesa mtandoni bila hata kuwa na website. Unaweza kusoma hapa kujua hatua za kupata pesa bila kuwa na tovuti, pia zipo njia nyingine nyingi ambazo unaweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia tovuti hii, unacho takiwa kufanya ni kujiunga kwa kutumia link hapo chini kisha utaweza kuona njia mbalimbali za kuweza kujipatia pesa mtandaoni.

Bofya Hapa Kujiunga na Propeller Ads

Na hizo ndio tovuti 6 ambazo unaweza kuzitumia kupata pesa mtandaoni, kumbuka kila tovuti hapa inahitaji bidii ili uweze kutengeneza pesa kwa haraka, kama ulikuwa unatafuta njia rahisi ya kutafuta pesa mtandaoni basi unaweza kusoma makala zetu nyingine kwenye kipengele cha Pesa mtandaoni.

9 comments
  1. jinsi ya kupata app ya top buzz link yake na hile ya kutengeneza qr code na taharf za tanzania kwa ufupi nihitaji nisaidie hizo links tafadhari

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use