Tovuti ya Muziki ya What.cd ambayo inatumia mfumo wa Torrent hivi karibuni imefungwa na serikali ya ufaransa kwa kuvunja sheria ya hati miliki kwa kusambaza miziki mbalimbali kinyume na sheria.
Tovuti ya What.cd ilianzishwa mwaka 2007 baada ya tovuti nyingine ya muziki ya torrent Oink kufungiwa hapo mwaka 2007. Tovuti ya Oink ilifanikiwa kuwa hewani kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 na kufungiwa rasmi na kupelekea tovuti ya What,cd kuzaliwa rasmi mwaka huohuo 2007. Hata hivyo tovuti ya What.cd ambayo ilikua na Server zake zaidi ya 12 imeondolewa rasmi hapo juzi ambapo kwa sasa tovuti hiyo haipo kabisa.
Mwanzoni baada tu ya kufungiwa tovuti hiyo iliandikwa kwenye ukurasa wake wa mwanzo kuwa tovuti hiyo imeondolewa kabisa na hakutakua na uwezekano wa tovuti hiyo kurudishwa tena kwenye mtandao. Hii ni mara ya tatu sasa kwa mwaka huu kwa tovuti za torrent kufungiwa kutokana na kuvunja sheria za haki miliki, kwani mapema mwaka huu tovuti maarufu ya Kickass torrent nayo ilifungiwa na kufuatiwa na tovuti nyingine ya Torrentz zote zikiwa zinatumia mfumo wa torrent.
Kwa taarifa zaidi za kuhusu tovuti hizi na nyingine nyingi endelea kutembele tovuti ya Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.