Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafuatilia tovuti ya Tanzania tech basi lazima utakua unajua kuwa tunayo list ya app nzuri ambazo huwa tunazitoa kila mwezi mara moja.
Kwa siku ya leo nitaenda kuanza list mpya ambayo tutakuwa tuna angalia website nzuri ambazo zinaweza kukusaidia kurahisisha mambo mbalimbali kwa haraka na urahisi. Kwa siku ya leo nimekuleta list hii yenye tovuti au website za kuelimisha, kuburudisha na kurahisha mambo.
TABLE OF CONTENTS
- 1 Tafuta Vitabu Matumizi
- 2 Angalia Internet Yako Ina Kasi Gani
- 3 Tafuta PDF Yoyote
- 4 Tuma Meseji Zinazojifuta
- 5 Edit PDF bila Programu Yoyote
- 6 Edit Picha Yoyote kwa Urahisi
- 7 Moyo Wako Umedunda Mara Ngapi Toka Kuzaliwa
- 8 Ondoa Background Kwenye Picha
- 9 Tengeneza Post za Instagram
- 10 Fahamu Bei ya Simu Yoyote Tanzania
- 11 Tengeneza App Bila Ujuzi Wowote
- 12 Buni Muonekano wa Bidhaa Zako
Tafuta Vitabu Matumizi
Manualslib ni website itakayo kusaidia kupata kitambu cha matumizi cha bidhaa yoyote, kama ulinunua bidhaa yoyote na ukapoteza kitambu kinacho onyesha jinsi ya kutumia basi tovuti hii inaweza kukusaidia sana kupata user manual za bidhaa mbalimbali, ambazo hujui kuzitumia kwa namna moja ama nyingine.
Angalia Internet Yako Ina Kasi Gani
Kama unataka kujua uwezo wa internet yako basi fast ni tovuti bora kwako, tovuti hii ni tofauti na tovuti nyingine ambapo hii inaweza kukupa data za ukweli kwa asilimia kubwa. Tovuti hii inamilikiwa na neflix na haina matangazo hata kidogo.
Tafuta PDF Yoyote
Kama unataka kupata PDF ya aina yoyote iwe kitabu au kitu chochote ambacho unahisi kitakuwa kwenye mfumo wa PDF basi tovuti hii itakusaidia sana. Kupitia tovuti hii utaweza kutafuta Vitabu, mafile ya aina mbalimbali, ripoti, vitabu vya shule na doc yoyote ambayo itakuwa kwenye mfumo wa PDF. Kama wewe ni mwanafunzi tovuti hii ni muhimu zaidi kwako.
Tuma Meseji Zinazojifuta
Privnote ni tovuti nyingine nzuri ambayo inaweza kukusaidia kutuma meseji ya siri ambayo inaweza kujifuta. Kama unataka kushare na mtu kitu na unataka kitu hicho kisiweze kuonekana tena basi tumia tovuti hii, andika meseji kisha bofua create not na utapata link maalum kisha share na unaetaka apate note hizo.
Edit PDF bila Programu Yoyote
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafanya kazi kwenye ofisi au unatumia PDF sana basi tovuti hii ni bora sana kwako, kupitia tovuti hii utaweza kuedit pdf kwa urahisi na haraka na bure bila kulipia. Pia unaweza kutumia programu ya kompyuta kama unataka uwezo zaidi.
Edit Picha Yoyote kwa Urahisi
Kama unataka kuedit picha kwa namna ya kipekee bila kutumia programu yoyote basi tumia tovuti hii ya pixlr, tovuti hii ina uwezo kama ilivyo programu ya adobe na unaweza kuedit picha kwa urahisi na kwa uwezo wa hali ya juu.
Moyo Wako Umedunda Mara Ngapi Toka Kuzaliwa
You’re getting old ni tovuti ambayo itakusaidia kufurahia siku yako kwa kujua mambo mbalimbali kuhusu wewe au watu wako wa karibu. Tovuti hii itakwabia muda ni siku ngapi umeishi hadi sasa, moyo wako umedunda mara ngapi kuanzia umezaliwa hadi sasa na mambo mengine mengi kuhusu umri wako.
Ondoa Background Kwenye Picha
Tovuti hii ni moja kati ya tovuti bora sana ambazo zitakusaidia kuondoa background kwenye picha kwa urahisi na haraka, kitu cha muhimu ni kuwa na picha unayotaka kuondoa background kisha moja kwa moja bofya hapo chini na utaweza kuondoa background kwenye picha zako kwa urahisi na haraka.
Tengeneza Post za Instagram
Tovuti hii itakusaidia kutengeneza post zako za mitandao ya kijamii kwa urahisi na bure kabisa, tovuti hii ni rahisi kutumia na mtu yoyote anaweza kujiunga na kuanza kutengeneza post za mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Twitter pia unaweza kutengeneza kadi za mwaliko kwa urahisi na haraka kwa kutumia tovuti hii.
Fahamu Bei ya Simu Yoyote Tanzania
Kama wewe ni mtanzania na ulikuwa unataka kujua bei ya simu yoyote au laptop au smartwatch kabla ya kununua basi unaweza kutembelea tovuti hii, mbali ya kuona bei unaweza kuona sifa za bidhaa husika ikiwa pamoja na kulinganisha bei na sifa baina ya bidhaa moja na nyingine.
Tengeneza App Bila Ujuzi Wowote
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa wanataka kutengeneza app yako pekee basi tovuti hii itakusaidia kufanya hivyo kwa urahisi, kupitia tovuti hii utaweza kutengeneza app kwaajli ya biashara app kwaajili ya blog yako pamoja na mambo mengine kama vile app ya YouTube na mengine kama hayo, pia utaweza kuweka app yako Play Store.
Buni Muonekano wa Bidhaa Zako
Kama wewe ni mmoja watu ambao wanauza bidhaa mbalimbali kama nguo au vitu vingine basi unaweza kutumia app hii kuweza kuangalia muonekano wa bidhaa zako kwa urahisi, unaweza kutengeneza mockup za bidhaa mbalimbali kama T-shirt, vikombe au hata apps na website pamoja na vifungashio vya bidhaa mbalimbali.
Na hizo ndio tovuti ambazo nimekukusanyia kwa siku ya leo, kama unataka kujua tovuti nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua tovuti za kubet kwa hapa nchini Tanzania. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.
Kazi nzuri jamani mnajitahidi sana
Asante na karibu sana
Ni nzuri sanaaa